Wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi Kidutani wamepatiwa huduma za Upimaji wa Afya na madaktari kutoka China

JUMLA ya watoto 400 wa Skuli ya Maandalizi ya Kidutani wamepatiwa huduma ya upimaji wa afya ili kuhakikisha wanakuwa na afya njema. Zoezi hilo lililofanyika skuli hapo, liliendeshwa na timu ya Madakari wa Kujitolea kutoka China ambapo watoto hao walipatiwa uchunguzi tofauti ikiwemo upimaji wa macho, masikio, vinywa na shinikizo la damu. Akizungumza kwenye zoezi […]

Wizara ya afya Zanzibar imekabidhiwa sehemu ya ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Jimbo la Magomeni

Wizara ya afya Zanzibar imekabidhiwa  sehemu ya ardhi   yenye ukubwa wa mita za mraba 1564.12 katika eneo la magomeni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha jimbo. Akizungumza katika makabidhiano hayo katika eneo la  kiwanja cha mpira wandarasi magomeni mkoa wa mjini magharibi, mkurugenzi mkuu wizara ya afya Zanzibar dr amour Suleiman mohammed […]

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itafanya jitihada za makusudi kuhakikisha mawasiliano yanafanyika kwa maabara zote za Afya nchini

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itafanya jitihada za makusudi kuona kuwa mawasiliano yanafanyika kwa maabara za Afya na maabara nyengine hapa nchini kwa lengo la kukabiliana na magonjwa mbali mbali yakiwemo ya miripuko. Akizungumza katika mkutano wa kupitia Muongozo wa Maabara kwa wadau mbali mbali, Mkurugenzi Tiba wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Marijan Msafiri […]

Wizara ya Afya Zanzibar imekabidhi kifaa cha kupumilia kinachojulikana kama Portable Oxygen kwa Bi Zahra Waziri Saidi

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Boharikuu ya Dawa Zanzibar(CMC) imekabidhi kifaa cha kupumilia kinachojulikana kama portable oxygen kwa Zahra Waziri Saidi anaesumbuliwa na ugonjwa wa kupooza viungo. Akikabidhi kifaa hicho naibu waziri wa afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh  amesema kuwa taarifa za kuhitaji kifaa hicho wamezipata kupitia mitandao ya kijamii na kuona ipo haja […]

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana saini mkataba na Global Fund wa ruzuku ya fedha za kupambana na Malaria, Ukimwi na Kifua Kikuu

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana saini mkataba na Mfuko wa Fedha wa Dunia (Global Fund) wa ruzuku ya fedha za kupambana na malaria, ukimwi na kifua kikuu wenye thamani dola milioni 11. Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa ZURA, ikishuhudiwa na watendaji kadhaa wa Serikali ya Zanzibar na Mwakilishi wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana […]

WIZARA ya Afya Zanzibar imewataka wananchi kuepuka matumizi ya dawa za kienyeji katika kutibu ugonjwa wa macho

WIZARA ya Afya Zanzibar imewataka wananchi kuepuka matumizi ya dawa za kienyeji katika kutibu ugonjwa wa macho ulioikumba jamii katika kipindi cha hivi karibuni. Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh, alisema, kufanya hivyo kunaweza kuongeza ukubwa wa tatizo hilo na kushauri wagonjwa kufika katika vituo vya afya ili kupata […]

Loading