Wizara ya Afya Zanzibar imekabidhi kifaa cha kupumilia kinachojulikana kama Portable Oxygen kwa Bi Zahra Waziri Saidi

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Boharikuu ya Dawa Zanzibar(CMC) imekabidhi kifaa cha kupumilia kinachojulikana kama portable oxygen kwa Zahra Waziri Saidi anaesumbuliwa na ugonjwa wa kupooza viungo.

Akikabidhi kifaa hicho naibu waziri wa afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh  amesema kuwa taarifa za kuhitaji kifaa hicho wamezipata kupitia mitandao ya kijamii na kuona ipo haja kumsaidia Zahra kutokana na umuhimu wa hitaji lake.

Alisema awali Zahra walimpatia kifaa kutoka bohari kuu ya dawa ambacho kinatumia umeme na wakati anapokitumia, hata hivyo kifaa hicho  kinatumika anapokuwa nyumbani tu na hawezi kutembea nacho.

Naibu waziri huyo ameitaka familia ya Zahra kukitunza kifaa hicho ili kiweze kudumu na kumsaidia  katika kipindi hiki cha maradhi yanayomsumbua na kuahidi kuwa Serikali ipo pamoja nae katika kumsaidia juu ya ugonjwa wake.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu Bohari kuu ya Dawa Abdulhalim Mzale amesema kuwa kifaa hicho kitakuwa mkombozi kwa Zahra pale anapotaka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Amefahamisha kuwa mashine hiyoinauwezo mkubwa wa kumsaidia  na  kwakipindi ambacho kuna tatizo la umeme kukatika kwani kifaa hicho kinauwezo wa kukaa chaji kwa zaidi ya saa 6.

Kwa upande wa Familia ya Zahra imeishukuru serikali kwa msaada huo na kuitaka serikali kuendelea kumsaidia matibabu katika wakati huu mgumu wa maradhi yanayomsumbua

Maradhi ya kupooza viungo yanayojulikana kitaalamu kama multiple sclerosis yanayoshambulia mfumo mkuu wa neva hayana tiba licha ya kuwa bado madaktari wanaendelea kuyafanyia utafiti duniani ili kubaini chanzo cha maradhi haya.

 

Loading