Wizara ya Afya imepokea msaada wa vifaa Tiba na dawa kutoka Marekani

WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa vifaa mbali mbali kutoka Taasisi Africa Relief and community Development ya Nchini marekani  na taasisi nyengine vyenye thamani ya Zaidi ya dola laki mbili. Akipokea msaada huo Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema vifaa hivyo ni vifaa ni vya   kuwasaidia wagonjwa waliolazwa, vifaa vya sehemu ya […]

Rais Mwinyi amewakumbusha wauguzi na watumishi wa sekta ya afya kuisaidia serikali kuleta Maendeleo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewakumbusha wauguzi na watumishi wote wa sekta ya afya kuendelea kuisaidia serikali katika kuhakikisha inatekeleza malengo yake ya kuwapatia huduma bora za afya wananchi wa Zanzibar bila ya ubaguzi. Dk.Mwinyi alieleza hayo katika kilele cha siku ya wauguzi duniani iliyofanyika katika ukumbi […]

Wizara ya Afya imefanya mazungumzo na kuagana na Balozi wa Norway ambae amemaliza muda wake nchini Tanzania

WIZARA Afya Zanzibar imesema itaendeleza ushirikiano na Norway katika kuimarisha Sekta ya Afya na wananchi wapate huduma zenye ubora. Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui alipofanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Elizabeth Jacobsen ambae amefika ofisini kwake kuaga kwa kumaliza muda wake. Waziri Mazrui amefahamisha Norway imeweza kuisadia Sekta […]

Baraza la Uuguzi na Ukunga limefanya ukaguzi Chuo cha Afya Cha Empirial kilichopo kisauni Zanzibar

Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Amina Abdulkadir amesema kuwepo kwa vyuo vyenye kukidhi vigezo vya kusomeshea fani ya uuguzi na ukunga hapa nchini kutasadia kutoa wataalamu wenye ubora wa kuhudumia wananchi. Amesema faini ya uuguzi na ukunga inahitaji taaluma yeye kiwago cha hali ya juu amayo itamuwezesha mwanafunzi kuwa na uwezo mkubwa […]

Chuo kikuu Cha haukland kujenga maabara ya kufundishia Zanzibar

CHUO kikuu cha Haukland  cha nchini Norway kinatarajia kujenga Maabara ya kufundishia hapa nchini ambayo itakuwa na uwezo wa kuwafundisha wanafunzi mbali mbali wa ndani na nnje ya nchi. Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Maabara hiyo itajengwa katika maeneo ya Lumumba na ujenzi wake utagharimu shilingi milioni mia nane na utachukua kipindi […]

Maadhimisho ya wiki ya maabara Duniani

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema, serikali itaendelea kuziimarisha maabara kwa lengo la kupata matokeo sahihi ya vipimo na tafiti za kimaabara nchini. Dk. Mwinyi, aliyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla katika mkutano wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya […]

Utoaji elimu juu ya huduma za maabara inahitajika kwa wananchi

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Abdulghulam Hussein, amesema, utoaji elimu juu ya matumizi sahihi ya huduma za maabara inahitajika kufikishwa kwa umma ili kujenga taifa lenye afya njema. Hayo aliyaeleza wakati akifungua maonyesho ya wiki ya maabara duniani huko viwanja vya Muembe Kisonge jana. Alisema, bado wananchi wengi wanashindwa kufahamu kazi […]