Wizara ya Afya Zanzibar imesema itafanya jitihada za makusudi kuhakikisha mawasiliano yanafanyika kwa maabara zote za Afya nchini

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itafanya jitihada za makusudi kuona kuwa mawasiliano yanafanyika kwa maabara za Afya na maabara nyengine hapa nchini kwa lengo la kukabiliana na magonjwa mbali mbali yakiwemo ya miripuko. Akizungumza katika mkutano wa kupitia Muongozo wa Maabara kwa wadau mbali mbali, Mkurugenzi Tiba wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Marijan Msafiri […]

Wizara ya Afya Zanzibar imekabidhi kifaa cha kupumilia kinachojulikana kama Portable Oxygen kwa Bi Zahra Waziri Saidi

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Boharikuu ya Dawa Zanzibar(CMC) imekabidhi kifaa cha kupumilia kinachojulikana kama portable oxygen kwa Zahra Waziri Saidi anaesumbuliwa na ugonjwa wa kupooza viungo. Akikabidhi kifaa hicho naibu waziri wa afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh ¬†amesema kuwa taarifa za kuhitaji kifaa hicho wamezipata kupitia mitandao ya kijamii na kuona ipo haja […]

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana saini mkataba na Global Fund wa ruzuku ya fedha za kupambana na Malaria, Ukimwi na Kifua Kikuu

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana saini mkataba na Mfuko wa Fedha wa Dunia (Global Fund) wa ruzuku ya fedha za kupambana na malaria, ukimwi na kifua kikuu wenye thamani dola milioni 11. Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa ZURA, ikishuhudiwa na watendaji kadhaa wa Serikali ya Zanzibar na Mwakilishi wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana […]

WIZARA ya Afya Zanzibar imewataka wananchi kuepuka matumizi ya dawa za kienyeji katika kutibu ugonjwa wa macho

WIZARA ya Afya Zanzibar imewataka wananchi kuepuka matumizi ya dawa za kienyeji katika kutibu ugonjwa wa macho ulioikumba jamii katika kipindi cha hivi karibuni. Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh, alisema, kufanya hivyo kunaweza kuongeza ukubwa wa tatizo hilo na kushauri wagonjwa kufika katika vituo vya afya ili kupata […]

MAJALIWA AZINDUA HOSPITALI YA WILAYA YA KASKAZINI B PANGATUPU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 11, 2024 amezindua Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini B Pangatupu iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja yenye uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya laki moja kwenye Shehia 31 wilayani humo. Akizungumza baada ya ufunguzi wa hospitali hiyo iliyogharimu shilingi Bilioni 6.7 Mheshimiwa Majaliwa amesema itasaidia kupunguza adha kwa wakazi wa […]

Timu ya Madaktari wa Upasuaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja wapatiwa ushauri wa namna ya Kutibu wagonjwa wa Saratani

DAKTARI Bingwa wa Upasuaji Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, Dk.Rashid Masoud, amewahimiza wananchi juu ya huduma mbali mbali za kimatibabu zinazotolewa kwenye hospitali hiyo. Ushauri huo aliutoa baada ya mkutano wa majadiliano kwa njia ya mtandao wa ‘zoom’ na jopo la madaktari bingwa wa Hospitali ya Jiangsu ya China yaliofanyika jana. Majadiliano hayo yalikuwa juu ya […]

Loading