Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ni miongoni mwa Idara muhimu ndani ya Wizara ya Afya Zanzibar. Kazi zake ni:
- Kusimamia vitengo na kuongoza majukumu yote ya idara.
- Kuhakikisha mahitaji yote ya Idara yanatayarishwa na kusimamiwa kwa wakati kwa mujibu wa maagizo ya serikali na maoni ya wadau.
- Kusimamia uandaaji mpango wa mwaka na mpango mkakati wa maendeleo wa muda wa kati wa wizara.