UTANGULIZI
Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto, lengo lake kubwa ni kuimarisha afya ya mama na mtoto na kupunguza vifo vya akina mama na watoto vitokanavyo na uzazi. Kazi za kitengo hichi zinachangia moja kwa moja katika kufikia Malengo endelevu ya Millennia, MKUZA III, na Dira ya Maendeleo ya 2020. Kitengo kinajumuisha vitengo vitatu, ambavyo ni:-
- Kitengo cha Afya Uzazi na Mtoto (RCH)
- Kitengo cha Chanjo za Watoto (EPI)
- Kitengo cha Afya ya Tiba ya Mjumuuisho ya maradhi ya watoto (IMCI)
Jumla ya vituo vya Afya 172 vinatoa huduma za chanjo Unguja na Pemba. Mpango wa chanjo Zanzibar kwa mwaka 2019 ilijipangia lengo la kuinua kiwango cha chanjo kufikia asilimia 95% kwa ngazi ya taifa na zaidi ya asilimia 90% katika wilaya zote Unguja na Pemba.Kitengo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa ndani na nje kimeweza kutekeleza kazi zifuatazo katika vituo vyote vyenye kutoa huduma ya afya ya uzazi na mtoto.
Huduma za Chanjo.
- Usambazaji wa majokofu mapya ya chanjo kwenye vituo vya Afya
- Kuendelea kutoa huduma za chanjo kwenye vituo vyote vya huduma za Afya ya uzazi na mtoto.
- Kusimamia usafirishaji na usambazaji wa chanjo pamoja na vifaa vya chanjo kwenye vituo vya Afya
- Kufanya tathmini ya kazi za chanjo kwa kipindi cha nusu mwaka
- Kufanya ufatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo
- Kufanya ufatiliaji wa kazi za chanjo katika wilaya na vituo vya afya.
- Kufanya kampeni shirikishi ya chanjo ya Surua Rubella
- Kuimarisha ufatiliaji wa magonjwa yanayokingwa kwa chanjo
Huduma za Matibabu ya magonjwa ya Watoto kwa Uwiano.
- Kutathmnini sababu za vifo vya mama na watoto wachanga katika ngazi ya kanda Unguja na Pemba.
IRCH Machapisho