Blog

Wizara ya Afya Zanzibar imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali ya China katika kutoa huduma mbali mbali za Afya

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali ya China katika kutoa huduma mbali mbali za Afya ikiwemo kuwafanyia uchunguzi wa maradhi ya saratani shingo ya kizazi. Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyaeleza hayo   katika Mkutano wa kupokea ripoti ya uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya kizazi iliyofanywa na madaktari kutoka […]

Hospitali ya Mnazi mmoja Kufanyiwa ukarabati kupitia mradi wa BADEA

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Hospitali ya Mnazimmoja inatarajiwa kufanyiwa ukarabati na utanuzi mkubwa kupitia mradi wa BADEA. Ujenzi wa Hopitali ya Mnazimmoja unatarajiwa kuanza mwezi wa April 2024 ambapo mwezi wa Januari itatangazwa tenda ya ujenzi huo ambao utachukua kipindi cha mwaka mmoja hadi kumalizika kwake ambao utahusisha Hospitali ya mnazimmoja, […]

Wizara ya Afya Zanzibar imesema Waste X project umewazezesha vijana wengi kujiajiri na kuweka mazingira kuwa safi

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema mradi wa kuzisarifu taka kuzigeuza kuwa thamani yaani Waste X project umewazezesha vijana wengi kujiajiri na kuweka mazingira kuwa safi pamoja kuweza kujitengenezea kipato na kufanikisha maisha yao. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Salim Slim katika mkutano wa kufunga mradi wa Waste X Project […]

Waziri Afya Zanzibar amesema Taasisi za kidini zina nafasi kubwa katika kuisaidia Serikali juu ya utoaji wa huduma za afya

Waziri wa   Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui   amesema kuwa Taasisi za kidini zinanafasi kubwa katika kuisaidia Serikali juu ya utoaji wa huduma za afya  kwa wananchi wake. Waziri Mazrui ameyaeleza hayo huko Hoteli ya Golden Tulip alipofungua mafunzo ya Uongozi kwa Viongozi wa Hospitali za KKKT yaliwashirikisha viongozi wa vituo vya Afya, wafanyakazi na washauri […]

Wizara ya Afya Zanzibar imetangaza rasmi kuwa maradhi ya vikope yameondoka Zanzibar.

WIZARA ya Afya Zanzibar imetangaza rasmi kuwa maradhi ya vikope yameondoka baada ya Shirika la Afya ulimwenguni WHO kuthibitisha kuwa ugonjwa huo sio tishio tena katika visiwa vya Unguja na Pemba. Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyasema hayo katika Mkutano wa kusherehekea na kuipongeza   Zanzibar kuweza kutokomeza maradhi ya vikope kutoka asilimia 11.4 […]

Taasisi ya NED kusaidia kufanya matibabu ya Magonjwa ya Kichwa, Uti wa Mgongo na Mishipa ya hisia katika Hospitali ya Mnazimmoja

WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema   Taasisi ya NED imeweza kusaidia kufanya matibabu ya magonjwa ya kichwa, uti wa mgongo  na mishipa ya hisia katika hospitali kuu ya mnazimmoja na hadi kufikia sasa zaidi ya kambi 200 zimefanyika na kufanikiwa kuwafanyia upasuaji zaidi wagonjwa elfu tatu. Akifungua mafunzo ya uchunguzi wa ubongo wa […]

WIZARA ya Afya Zanzibar kupitia Kitengo NCD kwa ushirikiano wa Madaktari kutoka China wameweka Kambi ya Uchunguzi wa Saratani ya shingo ya kizazi katika Hospital ya Mnazi Mmoja

WIZARA ya Afya Zanzibar kupitia Kitengo cha Maradhi yasiombukiza NCD kwa kushirikina na Serikali ya China jimbo la Jiangsu wanaendelea na kambi ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi inayofanyika katika Hospitali ya Mnazi mmoja. Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema katika kuimarisha afya za wananchi wa Zanzibar zoezi hilo la uchunguzi […]

Wizara ya Afya Zanzibar imetiliana saini mkataba na Serikali ya China ya kukabidhiwa mradi wa Hospitali ya Abdalla Mzee ya Mkoani Pemba

WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini mkataba na Serikali ya China ya kukabidhiwa mradi wa Hospitali ya Abdalla Mzee ya Mkoani Pemba baada ya kufanyiwa ukarabati Mkubwa na utanuzi wa Hopitali hiyo na Serikali ya China. Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema mradi huo ambao umeanza mwaka 2020   umehusisha kuongeza Majengo na kufanya […]

WIZARA ya Afya Zanzibar imekusudia kuimarisha mifumo yake ya uagizaji dawa vifaa tiba, usambazaji na uhifadhi wa dawa katika Bohari zake za  Unguja na Pemba

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema kuwa imekusudia kuimarisha mifumo yake ya uagizaji dawa vifaa tiba, usambazaji na uhifadhi wa dawa katika Bohari zake za  Unguja na Pemba kupitia wataalamu kutoka nchini Afrika ya Kusini kupitia Shirika la misaada la Marekani USAID. Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui alipokutana na kufanya mazungumzo […]