Idara ya Uuguzi na Ukunga ni idara ambayo imeundwa mwanzoni mwa mwaka wa 2023,  na Mh. Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi, hii ni baada ya kuona upo umuhimu mkubwa wa Idara hiyo kutokana na idadi kubwa ya watendaji wake katika mfumo mzima wa utoaji huduma za Afya, ili kuhakikisha Afya za wananchi zinaimarika wakiwemo wazee, wajawazito na watoto na jamii kwa ujumla, pindi wanapoenda kupata huduma katika vituo vya Afya, hospitali na hata majumbani yaani (Home Based Care).

Hivyo mnamo tarehe 30/01/2023 ilitangazwa rasmi kurugenzi ya Uuguzi na Ukunga katika Wizara ya Afya Zanzibar. Tunamshukuru sana na tunampongeza kwa maamuzi yasiyo na shaka ambayo yataleta mabadiliko makubwa.

Muundo wa Idara una divisheni kuu tatu (3) ambazo ni:

  1. Divisheni ya Uuguzi na Ukunga Unguja: kazi ya divisheni hii ni kusimamia kazi za huduma za Uuguzi, huduma za Ukunga pamoja na Maadili ya kazi na huduma kwa wateja.
  2. Divisheni ya Uuguzi na Ukunga Pemba: kazi za divisheni hii ni kusimamia huduma zote za uuguzi na ukunga kwa kisiwa cha Pemba
  3. Divisheni ya Viwango, Ubora na Utafiti: kazi za divisheni hii ni kusimamia mafunzo ya uuguzi na ukunga katika maeneo ya mafunzo ya kujiendeleza na maeneo ya mafunzo kazini (Onjob training), tafiti (Clinical Research) na machapisho ya uuguzi na ukunga.
  1. Kuimarisha ubora wa huduma za Uuguzi na Ukunga katika ngazi zote (za umma na binafsi)
  1. Kutoa ushauri wa kimkakati na kiufundi kwa serikali kuhusu huduma za uuguzi na ukunga ndani ya mfumo wa huduma za afya
  1. Kukuza ushahidi msingi (Evidence Based) na mazoezi sanifu (Standardized) ya Uuguzi na Ukunga
  1. Kuendeleza ushirikiano (Collaborative Partnership) na wadau muhimu katika ngazi za kitaifa, kikanda na kimataifa
  1. Kuratibu mafunzo ya kada ya Uuguzi na Ukunga pamoja na mafunzo ya kujiendeleza katika taaluma na kutoa huduma bora katika jamii

Dira

Kutoa Huduma bora za Uuguzi na Ukunga  zenye kiwango ya hali ya juu ikizingatia heshima ,huruma,Utu wa binaadamu na utofauti wa kitamaduni ili  kukidhi viwango vya afya  vya ndani kikanda na kimataifa

Dhamira

Kutoa maelekezo ya sera, miongozo na msaada ili kuwawezesha wauguzi na wakunga kuzingatia uwezo wa kitaaluma,uelewa na kujitolea katika kutoa huduma bora ambazo zinakidhi matarajio ya umma.

Upakuaji (Downloads) wa taarifa mbali mbali za Uuguzi na Ukunga hapa:-

  1. Dira na Dhamira
Loading