Utumishi na Uendeshaji

Lengo la idara ya Uendeshaji na Utumishi ni kuziwezesha Idara na vitengo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa kuweka na kudumisha mazingira mazuri ya kazi na kuhakikisha kuwepo kwa nyenzo bora na vyakutosha vya kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao.

Kusimamia masuala ya kiutumishi kama ajira kwa watumishi wapya, kushughulikia kupandishwa vyeo, kuthibitishwa kwa watumishi, kujenga uwezo wa watumishi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na mrefu ili kuwawezesha kupata sifa stahiki na kuongeza ujuzi ili kumudu majukumu yao na kuratibu masuala ya mikataba ya utendaji kazi kwa watumishi (OPRAS). Pamoja na kutunza taarifa za siri na bayana za Wizara na taarifa za majadala binafsi ya wafanyakazi.

Kuwahudumia viogozi wa kitaifa wastaafu kulingana na sheria ya mafao kwa viongozi wa kisiasa sheria namba 3 ya mwaka 1999. Pamoja na kutunza nyaraka za siri za Wizara na majadala binafsi ya viongozi wa Wizara na watumishi wote.

Loading