Wizara ya afya Zanzibar imekabidhiwa sehemu ya ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Jimbo la Magomeni

Wizara ya afya Zanzibar imekabidhiwa  sehemu ya ardhi   yenye ukubwa wa mita za mraba 1564.12 katika eneo la magomeni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha jimbo.

Akizungumza katika makabidhiano hayo katika eneo la  kiwanja cha mpira wandarasi magomeni mkoa wa mjini magharibi, mkurugenzi mkuu wizara ya afya Zanzibar dr amour Suleiman mohammed Amesema  kwa kukabidhiwa kiwanja hicho inaenda kutimiza adhma ya serikali ya  kuwasogezea karibu na makaazi  huduma  za afya wananchi ili kupunguza usumbufu wa upatikanaji wa huduma hizo.

Amesema kutokana ukubwa wa Jimbo  hilo na kuwepo na idadi kubwa ya watu kuna umuhimu mkubwa wa kupatikana kituo cha afya ambacho kitakwenda kukidhi mahitaji ya kusaidia huduma za afya katika ngazi chini pamoja na kuweza kuboresha mfumo wa rufaa ili mtu akipata tatizo la afya anze kupata huduma katika ngazi ya msingi

Pia amesema wizara ya afya inaendelea kuimarisha huduma katika ngazi ya msingi ili kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi wote .

Dr amour amemshukuru mwakilishi wa jimbo la magomeni Jamal Kassim pamoja na wazee shehia hiyo kuweza kuhakikisha wanapatiwa uhalali na haki ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya ambao unatarajiwa kuanza mnamo mwezi wa sita mwaka huu.

Mwakilishi wa jimbo la magomeni Jamal kassim amesema  eneo hilo limetengwa maalumu kwaajili ya kujengwa kituo cha afya ambacho kitaweza kutoa huduma zote za msingi ambacho pia kitakua na uwezo wa kutoa huduma za kulaza wagonjwa .

Jamal pia amemshukuru dk mwinyi kwa kuridhia kua wananchi wa jimbo la magomeni kua na kituo cha afya ambacho kitakua mkombozi kwa wananchi kuweza kupata huduma za afya.

Loading