SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana saini mkataba na Global Fund wa ruzuku ya fedha za kupambana na Malaria, Ukimwi na Kifua Kikuu

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana saini mkataba na Mfuko wa Fedha wa Dunia (Global Fund) wa ruzuku ya fedha za kupambana na malaria, ukimwi na kifua kikuu wenye thamani dola milioni 11.

Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa ZURA, ikishuhudiwa na watendaji kadhaa wa Serikali ya Zanzibar na Mwakilishi wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.

Akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Hamza Hassan Juma, alisema, fedha hizo zitasaidia kufikia lengo kuu la kutoa huduma enedelevu kwa jamii ya Wazanzibari.

Aliuhakikishia uongozi wa Global Fund, kwamba serikali itazisimamia kikamilifu fedha hizo na zitafanyiwa kazi iliyokusudiwa kama historia inavyoonyesha kwamba hakujatokea ubadhirifu kutoka mfuko huo tokea miaka ya nyuma.

“Nimejuulishwa kwa kipindi hichi cha mwaka 2024 hadi 2026, zaidi ya dola za Marekani milioni 10 zimetengwa kwa miradi hii ya maendeleo.

“Hizi ni fedha nyingi zitakazosaidia wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwani huduma za afya za Zanzibar hazina mipaka ya nchi”.

Mapema, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk.Amour Mohamed, alielezea mafanikio pamoja na maeneo yanayohitaji kuhusiana na kuhusiana na mwanendo wa maradhi ya malaria, ukimwi na kifua kikuuu.

Alisema, kwa upande wa malaria, bado imebakia na maambukizi yalio chini ya asilimia moja na hiyo ilitokana na ripoti ya utafiti w afya ya jamii ya mwaka 2022.

Hata hivyo, alisema, takwimu za malaria zinaonyesha kuna ongezeko la la wagonjwa, kwa mwaka 2023, wagonjwa 18,174 waliripotiwa ukilinganisha na mwaka 2022 wagonjwa walikuwa 4,557.

Kwa upande wa vifao, alisema, vimeongezeka kufikia 19 kwa mwaka 2023 ikilinganishwa na vifo vinne mwaka 2023.

Aliitaja changamoto zinazoikabili programu ya kumaliza malaria ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa yaliopelekea kuwa na mvua ndefu za vuli ambazo zilisababisha ongezeko la mazalia ya mbu.

Kwa upande wa kifua kikuu, takwimu zinaonyesha ongezeko la wagonjwa hao kutoka 1,074 mwaka 2020 hadi 1,135 mwaka 2023, ambapo idadi kubwa ya waathirika ni walikuwa wanaume wenye umri wa miaka 25 hadi 65.

Kwa upande wa ukimwi, alisema, kutokana na utafiti imebainika kuwa kuna watu 8,866 wanaishi na HIV (PLHIV) Zanzibar ambao wanapokea matibabu hadi Septemba 2023.

Hata hivyo, alisema, Zanzibar ina janga la HIV lenye mkusanyiko , hasa miongoni mwa makundi maalum.

Aliyataja makundi hayo ni wanaotumia dawa za kulevya kwa shindano 9.3%, wanaume wanaojamiiana na wanaume wenzao 11.4% na wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili yao 21.1%.

Mapema,Mwakilishi wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria, Morrison Lendem, aliihakikishia serikali kwamba mfuko huo utaendelea kushirikiana na Zanzibar kwenye mapambano ya kutokomeza magonjwa hayo

Loading