Blog

Wizara ya Afya Zanzibar kuimarisha Taasisi ya Utafiti wa Afya ZAHRI

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema kuwa inafanya jitihada ya kuimarisha Taasisi ya utafiti wa afya ZAHRI ili iweze kutoa taarifa za kisayansi ambazo zitasaidia udhibiti wa magonjwa wa binaadamu. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi utumishi uendeshaji Mwatoum Ramadhan Mussa katika mkutano wa mashirikiano kati ya Taasisi ya Taifa ya utafiti wa maradhi ya Binaadamu NIMRI na […]

WAZIRI wa Afya Zanzibar amewapongeza Madkatari kutoka Hospitl ya Muhimbili

WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kuja kwa madaktari kutoka Muhimbili kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuwapatia huduma wananchi wa Zanzibar wenye maradhi tofauti kwa ufanisi mkubwa. Amesema kutokana na kuwepo kwa wagnjwa wengi wenye maradhi tofauti hapa nchini yakiwemo maradhi ya mikojo na maradhi mengine ambayo yanatakiwa kupatiwa matibabu na kutokana na upungufu […]

Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili MOI zimeendesha kambi maalum za Upandikazi Goti

Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili MOI zimeendesha kambi maalum ya  kupandikiza goti na nyonga bandia ambapo zaidi ya wagonjwa 16 wamefanyiwa upasuaji katika kpindi cha siku tano. Kambi hiyo imefanyika ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano kati ya Hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja na […]

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Pharm Access kuimarisha huduma za Afya Zanzibar

WAZIRI wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, amesema wataendelea kushirikiana na shirika la Pharm Access ili kuona wanaendelea kuwapatia huduma wananchi za afya zinaimarika nchini na kuendelea kutolewa kwa wakati. Akizungumza katika uzinduzi wa vikundi vya wagonjwa wanaishi na magonjwa yasiyoambukizwa (NCD) katika jamii ikiwemo ya presha na kisukari hafla ambayo ilifanyika katika ukumbi wa […]

Jamii yatakiwa kutumia vituo vya afya kupata huduma

Naibu waziri wa afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh ameiataka jamii kufuata huduma katika vituo vya afya z ikiwemo huduma ya afya ya mama na mtoto. wito huo ameutoa huko Tumbatu katika makabidhiano ya kituo cha afya ya mama na mtoto mara baada ya kufanyiwa matengenezo na kuweka tanki la maji safi na salama na wahisani […]

Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar aweka jiwe la msingi la Kituo cha Afya cha Mama na Mtoto Kizimkazi Dimbani

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka madaktari na wahudumu wa afya nchini kujitahidi kutoa huduma bora kwa jamii ili juhudi za serikali za kusaidiana na wahisani wa maendeleo katika kimarisha huduma za afya ziweze kuleta tija zaidi kwa wananchi. Mhe. Othman ameyasema hayo huko Kizimkazi Dimbani mkoa wa Kusini […]

CBM waahidi kuendeleza misaada yao kwa Zanzibar

SHIRIKA LA Cristian blind Mission CBM limesema litaendeleza misaada yake kwa Zanzibar katika kuwafikia watoto wenye ulemevu wa kuona kwa kutoa huduma mbali mbali zikiwemo za elimu na afya ili waweze kufikia malengo yao ya kimaisha. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la CBM Tanzania Nesia Mahenge huko Skuli ya Kiswandui wakati ujumbe wa […]

Loading