WAZIRI wa Afya Zanzibar amewapongeza Madkatari kutoka Hospitl ya Muhimbili

WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kuja kwa madaktari kutoka Muhimbili kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuwapatia huduma wananchi wa Zanzibar wenye maradhi tofauti kwa ufanisi mkubwa.

Amesema kutokana na kuwepo kwa wagnjwa wengi wenye maradhi tofauti hapa nchini yakiwemo maradhi ya mikojo na maradhi mengine ambayo yanatakiwa kupatiwa matibabu na kutokana na upungufu wa wataalamu   madaktari kutoka muhimbili wameweza kusadia kuwapatia matibabu ya upasuaji.

Waziri Mazrui amefahamisha kuwa kazi kubwa walioifanya madaktari hao wameweza  kuokoa fedha ambazo zilikuwa zitumike kupatiwa matibabu wagonjwa katika Hospitali za Dar es Sallam na nnje ya nchi.

Amesema katika kufanikisha huduma za Afya Serikali kupitia Wizara ya Afya imeamua kubinafsha baadhi ya huduma ikiwemo huduma yaMaabara, Mionzi na wanampango kuimarisha huduma za mkojo ili wananchi wanapofika kupata huduma wazipate kwa haraka na bila ya usumbufu wowote.

Amewapongeza madaktari hao kuja kutoa huduma hapa nchini na kuwataka kuendeleza mpango wao huo  wa kuja Zanzibar kutoa huduma mara kwa mara ili wananchi wapate huduma hizo ambapo tayari Serikali imeshajenga Hospitali za Wilaya na Mkoa na zenye  na vyumba vya upasuaji na kutawezesha kutoa huduma kwa ufanisi wa hali ya juu.

Akiwasilisha Ripoti juu ya kambi iliyofanyika tarehe 2 mpaka tarehe 7 katika Hospitali ya Kivunge Dkt Ally Bayser ambae ni mtaalamu wa maradhi ya mikojo Kutoka Muhimbili amesema wameweza kuwafanyia uchunguzi watu 114 na waliweza kuwafanyia upasuaji ni 108 ambapo kati ya hao watoto 41 na watu wazima ni 67.

Amefahamisha kuwa waliweza  kufanya upasuaji wa tezi dume kwa wagonjwa 10 na kufanya upasuaji mengine ikiwemo ya maradhi ya ngiri (hania) ambapo alisema namba kubwa waliofanya upasuaji huo ni maradhi ya hania.

Nae Dkt Ramadhan Hamisi kutoka chuo Kikuu cha Muhimbili amesema wataendelea kutoa huduma hapa Zanzibar kwa lengo la kuwasadia wananchi wa Zanzibar sambamba na kutoa Elimu kwa wataalamu wa Zanzibar na wanafunzi wao katika chuo kikuu cha Muhimbili.

Loading