Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili MOI zimeendesha kambi maalum za Upandikazi Goti

Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili MOI zimeendesha kambi maalum ya  kupandikiza goti na nyonga bandia ambapo zaidi ya wagonjwa 16 wamefanyiwa upasuaji katika kpindi cha siku tano.

Kambi hiyo imefanyika ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano kati ya Hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja na Taasisi ya MOI wenye lengo la kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi karibu na wananchi.

Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Marzui amesema kambi hii ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ally Mwinyi la kuhkikisha wananchi wanapata huduma za kibingwa na kibobezi bila kulazimika kuzifuata huduma hizo Dar es Salaam au nje ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Dkt.Muhiddin Abdi Mahmoud amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Dkt. Hussein Mwinyi , Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui kwa usimamizi imara kwenye sekta ya Afya.

Pia, Dkt. Muhiddin amemshukuru Mkurugenzi Mtandaji wa MOI Prof. Abel Makubi kwa kuridhia kuanzisha ushirikiano na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar pamoja na kutuma jopo la madaktari bingwa wabobezi pamoja na wauguzi wabobezi kutoa huduma kwa wananchi za Tanzania visiwani.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Violet Lupondo amesema Taasisi ya MOI imekua ikitekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kuhakikisha huduma za kibingwa za MOI zinasogezwa karibu na wananchi ambapo kwa sasa huduma hizo zinapatikana katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuwapunguzi wananchi usumbufu wa kufuata huduma MOI Dar es Salaam.

Loading