Naibu waziri wa afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh ameiataka jamii kufuata huduma katika vituo vya afya z ikiwemo huduma ya afya ya mama na mtoto.
wito huo ameutoa huko Tumbatu katika makabidhiano ya kituo cha afya ya mama na mtoto mara baada ya kufanyiwa matengenezo na kuweka tanki la maji safi na salama na wahisani kutoka nchini Oman.
Amesema azma kubwa ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kupunguza vifo h vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga hivyo amewataka wananchi kuitumia kituo hicho ili kuondokana na matatizo mbali mbali yanayotokana na uzazi.
Ameyasema haya katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa ukarabati wa jengo la mama na mtoto na ujenzi wa mnara na uwekaji wa tank la maji safi. Aidha alifahamisha wizara ya afya inaendelea na mpango wa kuimarisha huduma na miundo mbinu ili kina mama waweze kujifungua salama.
Katika kufikia adhma ya serikali kutoa huduma bora za afya ameitaka DHMT kukiwezesha kutoa huduma za afya masaa 24 kwa huduma za uzazi.
Pia ametoa maelekezo kwa mkuu wa wilaya kupata mashirikiano ya moja kwa moja na kikosi cha ukozi KMKM katika huduma za usafiri wa boti ya huduma za dharura ili kuweza kupunguza hatari ya vifo vya mama na mtoto.
Amewashukuru wahisani wa Oman pamoja na Wafadhili wote wakiwemo PBZ,UFPA na Benjamin mkapa kwa kuendelea kutoa kusaidia katika sekta ya Afya katika kituo cha tumbatu gombani.
Mkurugenzi mkuu wizara ya afya zanzibar dr Amour suleiman mohd amewasisituza watendaji wa afya kutimiza wajibu katika kuitunza miundo mbinu ili kuweza kutoa huduma endelevu.
Ametaja miongoni mwa Vipaombele vya wizara ya afya ni kuimarisha huduma za msingi,kuimarisha mfuko wa fedha na
Kuweka huduma endelevu za upatikanaji dawa katika vituo vya afya mipango ambao itasaidia kupunguza vifo, magonjwa na kupugungza ghrama za matibabu
Amesema bado Kuna changamoto vifo vya mama na mtoto kutokana na Tafiti za 2022 zinaonesha Vifo vya mama wajawazito kati ya mama laki moja mia moja na kumi wanafariki wakati wa ujauzito ,wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.
Hivyo amewataka Watendaji wa vituo vya afya ya msingi kutoa huduma bora na kukikisha wanaweza kugundua Dalili hatar mapema ili kina mama waweze kujifungua salama.
Nae mkuu wa wilaya ya kaskazini unguja sadifa .ameipongeza wizara ya afya kwa kushirikiana na washirika katika kutekelza kwa vitendeo Ilani ya chama cha mapinduzi ya kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.
Nao wahisani kutoka oman waliosaidia katima ukarabati na uwekaji wa maji katika kituo hicho wameahidi kuendeleza mashirikiano katika kuisaidia wizara ya afya