WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kampuni ya ABE MWANGAZA CO LTD ya Dares Salaam kwa ajili ya kusaidia usafiri wa mama wajawazito wakati wanapokwenda kujifungua kupitia mradi wa Mmama.
Akipokea mchango huo Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema mchango huo uliotolewa utasaidia na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kuweza kuwahishwa mama wajawazito hospitalini kujifungua kupitia mpango maalumu uliokuwepo wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Amefahamisha kuwa mpango wa Mmama unahusisha kukusanya fedha ambazo husaidia upatikanaji wa usafiri wa kuwahishwa hospitalini kwenda kujifungua na lengo kubwa la mpngo huo ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Waziri Mazrui ametoa wito kwa wafanyabiashara, Makampuni na Taasisi mbali mbali kusaidia mpango wa Mmama kwa kuchangia fedha ambazo zitasaidia masuala mazima ya huduma za afya ya mama na mtoto hasa wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya ABE Mwangaza CO.LTD Eunice Bushanga amesema kuwa ameguswa vifo vinavotokea vya mama wajawazito na watoto wachanga na ameona ipo haja ya kusaidia pesa hizo kwa ajili ya usafiri kupitia Mradi wa Mmama.
Katika hatua nyengine Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka jumuiya ya Aster DM Healthcare ya nchini Dubai ambao wanashughulika kutoa huduma kwa kutumia mobile kiliniki
Amesema ujumbe huo utawezesha kusadia Zanzibar katika kutoa huduma kwa njia ya mobile kiliniki kwa kupita sehemu mbali mbali Unguja na Pemba kutoa huduma za afya na wanatarajia kuanza kutoa huduma hizo mwezi wa kumi mwaka huu.
Amefahamisha kuwa mbali na huduma hizo pia watasaidia kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya Afya kwa kuwapatia mafunzo ili kuweza kutoa huduma bora za afya hapa nchini.
Kwa uapnde wa mwakilishi wa Ujumbe huo amesema wameona ipo haja ya kuja kutaoa huduma hizo za mobile kiliniki hapa nchini kwa lengo la kurahisha upatikanaji wa huduma hasa vijijini.
Amefahamisha huduma za mobile kiliniki zimeweza kufanikiwa katika nchi mbali mbali na zinasaidia kutoa huduma kwa ukaribu na wananchi husiuka .