Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Mazrui amepokea vifaa kutoka PBZ, Team Fei Toto na Team Bui

Waziri wa afya zanzibar Nassor Ahmed.Mazrui amepokea vifaa kutoka PBZ bank na team Fei Toto na Bui i kwa ajili ya akina mama na watoto. Vifaa hivyo muhimu ambavyo vitasaidia afya ya mama pamoja na watoto vimegharimu zaidi ya shilingi milioni tisa.

Waziri mazrui amesema bank ya PBZ inamchango mkubwa kwa Jamii inayoendelea kuitowa kwa taifa kupitia sekta zote ikiwemo ya afya, amewataka wananchi wa zanzibar na Watanzania kuendelea kuiunga mkono PBZ ili iweze kufanya vizuri zaidi na kupata nguvu ya kusaidia zaidi.
aidha amefahamisha kitendo walichokionesha vijana Fei Toto na Bui ni kizuri na kuwataka kuendeleza na kuweza kusaidia nchi yao
kwa upande wa katibu mkuu wa Wizara ya afya dkt Fatma Mrisho amesema Watashirikiana katika kusaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Loading