CBM waahidi kuendeleza misaada yao kwa Zanzibar

SHIRIKA LA Cristian blind Mission CBM limesema litaendeleza misaada yake kwa Zanzibar katika kuwafikia watoto wenye ulemevu wa kuona kwa kutoa huduma mbali mbali zikiwemo za elimu na afya ili waweze kufikia malengo yao ya kimaisha.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la CBM Tanzania Nesia Mahenge huko Skuli ya Kiswandui wakati ujumbe wa Shirika hilo ulipofanya ziara maalum ya kuangalia miradi inayofadhiliwa na Shirika hilo kwa kupitia Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja.

Amefahamisha Shirika la CBM ni Shirika la kimataifa  linalotoa huduma takriban nchi 41na  linasadia zaidi katika kutoa huduma za watu wenye ulemavu na kwa Zanzibar wanasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika skuli ya Kiswandui kwa kutoa vifaa na huduma nyengine.

Amesema kwa upande wa Skuli ya Kiswandi wameridhika na taaluma wanayoitoa kwa wanafunzi wa Skuli hiyo kutokana na kufanya jitihada kubwa wa kuwapatia taaluma pamoja na ushirikiano walionao kati ya walimu wanafunzi na wazazi.

Kwa upande wa mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kiswandui Ali Abdalla Mahmoud ameshukuru kwa misaada wanayopatiwa na Shirika la CBM na wanawezesha wanafunzi hao kusoma kwa ufanisi licha ya kuwa na mazingira magumu ya kufundishia kutokana na upungufu wa vifaa na walimu.

Amefahamisha kuwa kutokana na hali hiyo Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Taasisi nyengine wanafanya kila jitihada ya kuona wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanapatiwa elimu kama wanafunzi wengine.

Alisema kwa sasa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wanampamgo kwa kila Wilaya kuwe na Darasa Elimu ya wanafunzi wenye mahuitaji maalumu ili kuweza kuondokana na changamoto za kufuata elimu kwa masafa ya mbali.

Kwa upande wa wazazi wa watoto wenye mahitaji maalumu wamesema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya usafiri hivyo wameitaka Serikali kufanya jitihada ya kuwa na usafiri wao maalumu ya kuwapeleka na kuwarejesha skuli na kuepukana na matatizo ya kwenye daladala.

Katika hatua nyengine ujembe wa Shirika la CBM wamefanya mazungumzo na Waziri wa Afya na Viongozi wa Wizara Hiyo na kuahidi kuendelea kusaidia Sekta ya hya afya katika masuala mazima ya huduma za watu wenye ulemavu.

Na upande wa Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameuwelezea ujumbe huo kuwa wanazingatia katika masula mazima ya watu wenye ulemavu na katika hospitali kumi za Wilaya na moja ya mkoa wamezingatia watu wenye ulemavu.

Loading