Blog

Maadhimisho ya wiki ya maabara Duniani

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema, serikali itaendelea kuziimarisha maabara kwa lengo la kupata matokeo sahihi ya vipimo na tafiti za kimaabara nchini. Dk. Mwinyi, aliyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla katika mkutano wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya […]

Utoaji elimu juu ya huduma za maabara inahitajika kwa wananchi

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Abdulghulam Hussein, amesema, utoaji elimu juu ya matumizi sahihi ya huduma za maabara inahitajika kufikishwa kwa umma ili kujenga taifa lenye afya njema. Hayo aliyaeleza wakati akifungua maonyesho ya wiki ya maabara duniani huko viwanja vya Muembe Kisonge jana. Alisema, bado wananchi wengi wanashindwa kufahamu kazi […]

Wizara ya Afya itaendeleza mikakati yake kuhakikisha 0 malaria inafikiwa

NAIBU Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh, amesema, wizara hiyo inaendelea na mkakati wake wa kuhakikisha inaendelea kuongoza kufanya vizuri dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa malaria hapa Zanzibar. Hayo aliyaeleza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho ya siku ya malaria duniani, hafla iliyofanyika Mnazimmoja. Alisema, huku taifa likiadhimisha siku hii, hali ya […]

Wizara ya Afya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa ukarabati na utanuzi wa Hospitali ya Mnazi mmoja

WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini mkataba na mshauri elekezi wa Kampuni ya Al Abdulhadi Engineering Consultancy ya Kuweit  na mshirika mwenzawake Apex Engineering ya Tanzania kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa na utanuzi  wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Fatma Mrisho emesema kuwa ukarabati huo mkubwa unaotarajiwa kuanza […]

Waziri wa Afya akutana na Ujumbe wa GHC Hospitals kutoka India

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya Zanzibar, imesema itaendeleza jitihada zake za kuimarisha huduma za maradhi ya moyo hapa nchini kwa kuleta madaktari bingwa wa magonjwa hayo kutoka nchi mbali mbali ikiwemo India ili kuweza kufanya uchunguzi na kuwapatia matibabu wagonjwa wenye maradhi hayo.Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui alipofanya mazungumzo […]

Serikali ya Marekani kuimarisha huduma za Afya Zanzibar

SERIKALI ya Marekani kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya inakusudi kuimarisha huduma za afya hasa katika maeneo ya homa ya inni na Ukimwi na maradhi ya miripuko. Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kuja kwa uwekazaji    wa miradi huo  utasaidia  kuanzishwa kwa programu mpya ya mkataba ambayo […]

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikiana na washirika wa maendeleo kukuza sekta ya afya

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikiana na washirika wa maendeleo mbali mbali katika kueka miundombinu iliyobora ya sekta ya afya ili wananchi waweze kupata huduma Bora za afya. Hayo yameelezwa na Waziri wa afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui wakati alipofanya mazungumzo na ujumbe kutoka Enter Capital limited wa nchini Netherland ambao una Nia ya kuimarisha […]

Wizara ya Afya itaendelea kutoa huduma za afya ya uzazi kwa vijana

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya itaendelea kuwaekea vituo vya huduma rafiki kwa vijana ili kuweza kuwasadia katika kupata huduma za afya ya uzazi kwa ukaribu na kuweza kukabiliana na changamoto wanazokabiliana nazo. Wito huo umetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Mh.Nassor Ahmed Mazrui huko Bumbwisudi alipofungua kituo cha kutolea huduma za afya ya uzazi kwa […]

Loading