Wizara ya Afya itaendelea kutoa huduma za afya ya uzazi kwa vijana

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya itaendelea kuwaekea vituo vya huduma rafiki kwa vijana ili kuweza kuwasadia katika kupata huduma za afya ya uzazi kwa ukaribu na kuweza kukabiliana na changamoto wanazokabiliana nazo.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Mh.Nassor Ahmed Mazrui huko Bumbwisudi alipofungua kituo cha kutolea huduma za afya ya uzazi kwa vijana na kuwataka vijana kukitumia kituo hicho kwa kupata huduma.

Amesema  kutokana na changamoto zinazowakumba vijana juu ya masuala ya mbali mbali ya afya ya uzazi Wizara ya afya kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo mbali mbali wakiwemo UNFPA inahakikisha inawasogezea karibu vijana huduma ili waondokane na matatizo wanayokabiliana nayo.

Amefahamisha katika kuwapa umuhimu mkubwa vijana, Wizara ya Afya kwa kushirikiana UNFPA na wadau wengine imefanya juhudi mbali mbali za kuhakikisha kuwa vituo vingi vya aina hiyo vinafunguliwa Unguja na Pemba ambapo kwa sasa jumla ya vituo kumi na tatu zimefunguliwa.

Amewataka vijana wa Bumbwisudi na maeneo ya jirani kukitumia kituo hicho cha huduma rafiki kwa kupata huduma za afya za uzazi ambazo zinatolewa kwa usiri mkubwa.

Mkurugenzi Mkaazi wa UNFPA Tanzania Mark Bryan

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa UNFPA Tanzania Mark Bryan amesema Shirika lake litaendeleza kutoa huduma za afya hasa huduma za afya ya uzazi kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema huduma rafiki kwa vijana na jambo la msingi kutokana vijana anaweza kujilinda na mambo yanayopelekea kuharibu afya zao na kuwataka vijana kujiepusha mambo yanayopelekea kuhatarisha afya.

Nae kaimu Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A Hamida Mussa amesema kuwa shehia ya Bumbwisudi imekuwa na vijana ambao wamekatisha masomo yao  na wamefanya utaratibu wa kuwarejesha maskulini.

Aidha alifahamisha kuwa katika Wilaya hiyo bado kuna idadi ya  vijana ambao wamepoteza dira ya maisha yao na  wasipoangaliwa vizuri wanaweza kuhatarisha maisha yao ambapo kwa kufunguliwa kwa kituo hicho kitawasadia katika kupata huduma na kuwaelekeza mustakbali wa maisha yao.

Loading