Wizara ya Afya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa ukarabati na utanuzi wa Hospitali ya Mnazi mmoja

WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini mkataba na mshauri elekezi wa Kampuni ya Al Abdulhadi Engineering Consultancy ya Kuweit  na mshirika mwenzawake Apex Engineering ya Tanzania kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa na utanuzi  wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Fatma Mrisho emesema kuwa ukarabati huo mkubwa unaotarajiwa kuanza hivi karibuni utagharimu shilingi bilioni mia moja fedha ambazo ni mkopo kutoka Kuweit, Fund Saud Fund na BADEA.

Amefahamisha mkataba huo utahusisha kufanyika kwa upenduzi yakinifu, kuandaa michoro, kufanya mchanganuo pamoja na gharama za ujenzi, nyaraka za kumtafuta mzabuni na kuandaa sifa za vifaa tiba ambao utachukua kwa kipindi cha miezi minane.

Aidha alisema ni mategemeo ya Wizara ya Afya kuwa hospitali hiyo itakapomalizika itakuwa Hospitali kubwa kwa Afrika Mashariki na itatumika kwa magonjwa ambayo yanahitaji ubingwa wa hali ya juu.

Alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya inafanya jitihada ya kukamilisha ujenzi wa Hospitali za Wilaya na Mkoa iliyopo Lumumba na kuhakikisha  kila mkoa inakuwa na Hospitali yake ili kuweza kuwahudumia wananchi kwa ufanisi wa hali ya juu.

Loading