SERIKALI ya Marekani kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya inakusudi kuimarisha huduma za afya hasa katika maeneo ya homa ya inni na Ukimwi na maradhi ya miripuko.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kuja kwa uwekazaji wa miradi huo utasaidia kuanzishwa kwa programu mpya ya mkataba ambayo itafanya kazi baina ya CDC ya Marekani na Wizara ya Afya na utaanzia kwa maradhi ya Ini Ukimwi na maradhi ya miripuko.
Amefahamisha mkataba huo utakuwa na vipengele mbali mbali vya kuimarisha huduma za afya hapa nchini ikiwemo masula mazima ya mifumo pamoja kuondoa maradhi ya mripuko, maradhi ya kuambukiza na mradi huo utakuwa wa miaka mitano katika utekelezaji wake.
Aidha alisema kwa muda wa miezi miwili kutoka sasa Wizara ya afya wanaandaa timu ya kutekeleza programu ya miezi saba itafanya mipango ya programu hiyo ambayo itatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na wananchi wa Zanzibar wataweza kufaidika nayo.
kwa upande wa ujumbe huo wamesema mradi huo mpya utakaoekezwa hapa nchini una nia ya kutomeza maradhi mbali mbali yakiwemo ya mripuko na utafanyika kwa mashirikiano makubwa baina ya CDC na Zanzibar.