WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kuwa utoaji wa mimba usiosahihi unaweza kusababisha madhaara mbali mbali ikiwemo kupata saratani na kuengeza idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi hapa nchini.
Akizundua dawa na kifaa maalumu cha kusafishia mji wa mimba sambamba na mafunzo kwa wataalamu wa sekta ya afya waziri Mazrui amesema Taasisi ya dkt international Tanzania itawezesha katika kuwapa huduma zilizobora kwa akinamama hapa nchini.
Amesema ni muhimu mimba zitolewe kwa njia zilizosahihi na iliobora ili mama akichukua mimba baadae asiathirike, Na Wizara ya afya isipate gharama ya kuwatibu akina mama ambao walitoa mimba kwa njia isiyo sahihi.
Amefamisha kuwa Wizara ya afya haipendi watu watoe mimba bila ya sababu ya msingi lakini kunasababu mbali mbali zinazopelekea utoaji wa mimba zikiwemo za ugojnwa hivyo, dkt international Tanzania imeleta dawa na kifaa ili kuweza kina mama kuwasadia kuwa katika hali ya usalama.
Amesema Wizara ya Afya kupitia Wakala wa chakula na dawa ZFDA imejiridhisha na dawa hizo pamoja na kifaa ya usafishaji wa mji wa mimba zilizozinduliwa na Taasisi ya dkt international Tanzania na wataweza kuzitumia kwa hospitali na vituo vya afya zilizoanishwa kutoa huduma hiyo.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Kinga na Elimu ya afya Zanzibar Dkt Fatma Kabole amesema bado vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga ni tatizo hapa nchini na Wizara ya afya kupitia wadau mbali mbali wanafanya jitihada ya kuondosha tatizo hilo.
Amesema vifo kwa akinamama vimepungua kidogo lakini kwa uapande wa watoto wachanga vinaendelea kutoa kila siku na wizara kupitia hadumu wa afya inafaatilia vifo hivyo ili kuweza kuondosha vifo hivyo na kuwataka vijana kuondokana na tabia ya kutoa mimba kiholela ili kuondokana na matatizo hayo.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa DKT International Tanzania Kevin Hudson amesema wamesajiliwa kutoa huduma hiyo Tanzania na wameona waje Zanzibar ili kuweza kusaidia upatikanaji wa huduma salama ya utoaji wa mimba ili wananchi wasipate madhara na kuweza kupunguza vifo vitonavyo na uzazi.
Amesema wameweza kusadia watu mbali mbali duniani ikiwemo Tanzania kwa utumiaji wa dawa hizo pamoja hivyo kwa Zanzibar wataweza kufaidika na kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.
Nae Afisa Masoko wa Taasisi ya DKT international Tanzania Deogratus kitama lengo la kuja Zanzibar uzinduzi na mafunzo maalum kwa ajili bidhaa za afya ya uzazi kwa ajili ya kupunguza zifo vitokanavyo na uzazi
Amesema bidhaa ya Vidonge vya ma-kare na na kifaa cha usafishaji wa mji wa mimba MVA plus vinatumika kimataifa na viko salama kwa asilimia 95 wa ufanisi matumizi yake na lengo kuwafikia wazanzibari na zitapatikana kwa sehemu ambazo zimesajiliwa kutoa huduma hiyo