Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikiana na washirika wa maendeleo kukuza sekta ya afya

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikiana na washirika wa maendeleo mbali mbali katika kueka miundombinu iliyobora ya sekta ya afya ili wananchi waweze kupata huduma Bora za afya.

Hayo yameelezwa na Waziri wa afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui wakati alipofanya mazungumzo na ujumbe kutoka Enter Capital limited wa nchini Netherland ambao una Nia ya kuimarisha sekta ya afya hapa nchini.

Amesema kutokana na sekta ya afya kuwa na Miradi mbali mbali ambayo inahitajika kutekelezwa ikiwemo ya miundo mbinu ya Afya na vifaa kwa mwaka huu 23 mpaka 25 watawapatia na kuona wanasaidia katika nyanja tofauti.

Kwa upande wa ujumbe huo umesema wameweza kutekeleza miradi kwa nchi mbali mbali hivyo kwa Zanzibar watasaidia kuimarisha sekta hiyo.

Loading