MAJALIWA AZINDUA HOSPITALI YA WILAYA YA KASKAZINI B PANGATUPU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 11, 2024 amezindua Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini B Pangatupu iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja yenye uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya laki moja kwenye Shehia 31 wilayani humo. Akizungumza baada ya ufunguzi wa hospitali hiyo iliyogharimu shilingi Bilioni 6.7 Mheshimiwa Majaliwa amesema itasaidia kupunguza adha kwa wakazi wa […]

Timu ya Madaktari wa Upasuaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja wapatiwa ushauri wa namna ya Kutibu wagonjwa wa Saratani

DAKTARI Bingwa wa Upasuaji Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, Dk.Rashid Masoud, amewahimiza wananchi juu ya huduma mbali mbali za kimatibabu zinazotolewa kwenye hospitali hiyo. Ushauri huo aliutoa baada ya mkutano wa majadiliano kwa njia ya mtandao wa ‘zoom’ na jopo la madaktari bingwa wa Hospitali ya Jiangsu ya China yaliofanyika jana. Majadiliano hayo yalikuwa juu ya […]

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itaendelea kuimarisha huduma mbali mbali kwa wazee wa Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itaendelea kuimarisha huduma mbali mbali kwa wazee wa Unguja na Pemba ikiwemo huduma za afya mahospitalini. Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh ameyasema hayo wakati alipofungua mkutano wa mwaka wa kutathmini masuala ya afya kwa wazee kupitia mradi wa maradi wa kuimarisha mazingira […]

RAIS wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema serikali inawatambua rasmi, wahudumu wa afya ya jamii (CHW) kama wafanyakazi wa afya ya jamii

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema serikali inawatambua rasmi, imewapokea kwa mikono miwili na itawaendekeza kwa kuwakuza katika fani hiyo mpya ya “Community Health Workers” wahudumu wa afya ya jamii kama wafanyakazi wa afya ya jamii . Dk. Mwinyi alieleza hayo wakati akizindua program hiyo ya kitaifa ya […]

Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi anatarajiwa kuzindua Programu ya Kitaifa ya Wahudumu wa Afya wa Kujitolea Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuzindua program ya kitaifa ya wahudumu wa afya wa kujitolea ili kutilia mkazo katika kuwatambua rasmi, kuwajengea uwezo kitaalamu na kuwawekea mazingira wezeshi ya utendaji kazi. Akitoa taarifa jana kwa waandishi wa habari huko katika ofisi za Wizara ya Afya Mnazimmoja, […]

Wizara ya Afya Itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kupunguza ongezeko la Ugonjwa wa Saratani

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikiana na Taasisi mbali mbali za ndani na nnje ya nchi   kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa ugonjwa wa saratani haundelei kuwaathiri wananchi wa Zanzibar. Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyaeleza hayo huko ofisi kwake wakati alipofanya mazungumzo na ujumbe kutoka Taasisi ya Saratani ya ocean Road wenye […]

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikina na Taasisi Uniting to Combat Neglected Tropical Disease

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikina na Taasisi inayoshughulikia Maradhi yasipewa kipaumbele ya nchini Ungereza Uniting to Combat Neglected Tropical Disease katika kuisaidia Zanzibar kupambana na maradhi hayo. Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inyoshughulikia maradhi yasiyopewa kipaumbele ya nchini Uengereza Bi. Thoko Elphick […]

WIZARA ya Afya imesema itaendelea kushirikiana na Serikali ya China katika kuimarisha afya za wananchi wake

WIZARA ya Afya imesema itaendelea kushirikiana na Serikali ya China katika kuimarisha afya za wananchi wake. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya, Dk.Salim Slim, alipokuwa akifungua zoezi la upimaji wa afya kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), zoezi lililoendeshwa na timu ya madaktari kutoka China. Alisema, upimaji […]

Wizara ya Afya Zanzibar imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali ya China katika kutoa huduma mbali mbali za Afya

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali ya China katika kutoa huduma mbali mbali za Afya ikiwemo kuwafanyia uchunguzi wa maradhi ya saratani shingo ya kizazi. Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyaeleza hayo   katika Mkutano wa kupokea ripoti ya uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya kizazi iliyofanywa na madaktari kutoka […]

Loading