Wizara ya Afya Itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kupunguza ongezeko la Ugonjwa wa Saratani

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikiana na Taasisi mbali mbali za ndani na nnje ya nchi   kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa ugonjwa wa saratani haundelei kuwaathiri wananchi wa Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyaeleza hayo huko ofisi kwake wakati alipofanya mazungumzo na ujumbe kutoka Taasisi ya Saratani ya ocean Road wenye lengo la kuimarisha huduma kwa Zanzibar.

Amesema ugonjwa wa saratani umekuwa ukiongezeka siku hadi siku kwa mwaka huu Wizara ya Afya Zanzibar imepeleka wagonjwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo wagonjwa 118 wapya wamepelekwa Taasisi ya Ocean Road.

Amesema kutokana na kuwepo kwa ongezeko la ugonjwa wa Saratani hapa nchini Wizara ya Afya inaendelea kufanya jitihada ya kukinga ugonjwa huo usiendelee kuathiri jamii kwa vile u si wa wakuambukiza ni ugonjwa ambao unasababishwa na vichecheo vingi ikiwemo kubadilisha mtimbo wa maisha wa kula vyakula vyenye mafuta mengi, utumiaji wa chumvi nyingi na kutofanya mazoezi.

Amefahamisha kuwa Wizara ya afya itaendelea kutoa Elimu kwa wananchi kupitia mradi wa  kinga dhidi ya saratani wenye lengo la kuwakinga wananchi wa Zanzibar ugonjwa wa saratani ambazo kwa hapa Zanzibar saratani ya shingo ya Kizazi, saratani ya matiti na tezi dume kwa wanaume ndizo zinaoongoza kuwaatahiri watu wengi hapa nchini.

Kwa upande wake daktari bingwa wa Saratani na   Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Taasisi ya Ocean Road Mark Athumani Mseti amesema wameona ipo haja ya kuishirikisha Zanzibar katika mradi wa kukabiliana na ugonjwa wa saratani nchini Tanzania ambao umekuwa ukiendelea kuathiri jamii.

Amesema taasisi ya Ocean Road imekuwa ikipokea wagonjwa wengi kutoka Zanzibar ikilinganishwa na idadi ya wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba ambapo alisema kupitia mradi wa kinga dhidi ya saratani na asilimia 90 ya uekezaji itakuwa katika kinga kwa ugonjwa wa saratani na Zanzibar itakuwa sehemu ya mfano kwenye mradi huo.

Kwa upande Dkt. Zomola kutoka taasis ya NGEZI amesema wanatamani idadi ya wagonjwa wa saratani inapungua kwa kiasi kikubwa nnchini Tanzania na mradi huu utawezesha kukinga na nguvu kazi ya taifa kuimarika.

Katika hatua nyengine Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amekutana na ujumbe kutoka BADEA kuzungumnzia masuala mazima ya kuanza kwa ukarabati na utanuzi wa hospitali ya Mnazimmoja ambapo ujenzi wake utaanza rasmri mwanzoni mwa  mwaka 2024.

Amesema fedha za mradi wa ukarabati na utanuzi wa Hospitali ya mnazimmoja zinatokana na mkopo kutoka BADEA ukushirikiana na mfuko wa Quiet na mfuko wa Saudi arabia na kuweza kupata karibu dola milioni 45   na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeingiza dola milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa hoispitali ya manzimmoja.

Mazungumzo na ujumbe huo yamejuisha juu ya masuala mazima ya utangazaji tenda wa kwa ajili ya mjenzi wa hospitali hiyo ambapo itakapokamilika  itakuwa kwa ajili ya maradhi ya kibingwa.

Loading