SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itaendelea kuimarisha huduma mbali mbali kwa wazee wa Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itaendelea kuimarisha huduma mbali mbali kwa wazee wa Unguja na Pemba ikiwemo huduma za afya mahospitalini.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh ameyasema hayo wakati alipofungua mkutano wa mwaka wa kutathmini masuala ya afya kwa wazee kupitia mradi wa maradi wa kuimarisha mazingira kwa ajili ya  uzee wenye afya.

Amesema Wizara ya afya tayari imeimarisha huduma kwa wazee katika hospitali mbali mbali na vituo vya afya pamoja na kuwaekea mahitaji muhimu ikiwemo madawa ili kuweza kuondokana na maradhi mbali mbali yakiwemo maradhi yasiombukiza NCD.

Amefahamisha kuwa Wizara ya Afya itafanya jitihada kwa wazee wanapofika mahospitali na Vituo vya Afya kupata huduma kwa urahisi na wsiweze kupata usumbufu wa kupata matibabu,

Amesema kuna baadhi ya wafanyakazi wa Mahospitalini hawatoi huduma nzuri kwa wazee na kuwafanya baadhi ya wazee na wananchi wengi wanaokwenda kupata huduma kukosa Imani na kukikmbilia hospitali nyengine zikiwemo za Tanzania bara, hivyo amesema kutokana na hali hiyo amewataka kubadilika kiutendaji na kuweza kutoa huduma nzuri.

Kwa upande wa Katibu wa Jumuiya za wazee Zanzibar JUWAZA Salama Kombo amesema kuwa kutokana na mapungufu na shida wanayoipta wazee katika kupata afya bora wanaendelea kupanga mambo mengi lakini ili kuweza kupata huduma bora za afya.

Amefahamisha kuwa jumuiya ya wazee na wastafu wameomba mradi huu maalumu ambao umetekelezwa kunazia mwaka 2022 na utafika disemba mwaka 2024 na kuweza kuwafahamisha wazee juu maradhi yasiombukiza ambayo yamekuwa ni tatizo la kidunia kutokana na kubadilisha mtindo wa maisha.

Kwa upande wake Afisa Afya na tathmini kutoka Help Age Martha Jerome amesema kuwa lengo la mkutano huo kushirikisha mbinu bora zilizotumika katika utekelezaji wa mradi ili kuendeleza katika mipango na afua mbali mbali.

Amesema malengo mengine ni kuandaa mpango wa utekelezaji wa mambo mbali mbali ikihusisha mbinu bora na kuona namna ambavyo vitajumuisha katika mipango ya utekelezaji na sera mbali mbali.

Nae Meneja wa Maradhi yasiombukiza Zanzibar Dkt Omar Mohamed Suleman amesema kupitia Kitengo cha Maradhi yasiombukiza wameandaa mkakati maalumu kuwakeza  katika masuala ya wazee wa kupata huduma za afya

Loading