DAKTARI Bingwa wa Upasuaji Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, Dk.Rashid Masoud, amewahimiza wananchi juu ya huduma mbali mbali za kimatibabu zinazotolewa kwenye hospitali hiyo.
Ushauri huo aliutoa baada ya mkutano wa majadiliano kwa njia ya mtandao wa ‘zoom’ na jopo la madaktari bingwa wa Hospitali ya Jiangsu ya China yaliofanyika jana.
Majadiliano hayo yalikuwa juu ya namna ya kumpatia matibabu mgonjwa anayekabiliwa na saratani ya utumbo mkubwa ambaye amelazwa kwenye hospitali hiyo.
“Tulikuwa tunataka ushauri wa kitaalamu wa njia gani nzuri zaidi ya kumtibu mgonjwa huyu, ikizingatiwa wenzetu wamepiga hatua kubwa”.
“Vikao hivi ya ushauriano ni vizuri kwa sisi madaktari na wagonjwa wetu, lango likiwa kutoa matibabu bora zaidi”
Alisema, majadiliano kama hayo yanafanyika kwa madaktari wa hapa hapa nchini, lakini, hilo lililofanyika ni kutokana na aina ya tatizo na kutokuwepo kwa mtalaamu wa moja kwa moja nje ya madkatari waliopo.
Alisema, baada ya ushauriano huo mgonjwa huyo ataanza kwa kupatiwa matibau ya kutumia dawa na baada ya miezi mitatu anatarajiwa kufanyiwa upasuaji.
“Tunapotaka ushauri wa daktari bingwa wa nchi nyengine, tunaokoa hata fedha kwa sababu huyo mgonjwa hatosafirishwa.
“Hili tulilolifanya si kwa kesi hii iliyotokea, lakini,
Naye Mkuu wa Madaktari kutoka China, Profesa Jiang Guoqing, alielezea matarajio yake ya kuendelea kwa ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya afya Zanzibar.
Aidha, aliishukuru Wizara ya Afya na Serikali kwa namna zinavyotoa ushirikiano mkubwa madaktari wa Kichina wanapofika Zanzibar kwa ajili ya kutoa huduma mbali mbali.