Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikina na Taasisi Uniting to Combat Neglected Tropical Disease

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itashirikina na Taasisi inayoshughulikia Maradhi yasipewa kipaumbele ya nchini Ungereza Uniting to Combat Neglected Tropical Disease katika kuisaidia Zanzibar kupambana na maradhi hayo.

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inyoshughulikia maradhi yasiyopewa kipaumbele ya nchini Uengereza Bi. Thoko Elphick Pooley aliyefika kujitambulisha.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya Zanzibar na washirika wa maendeleo mbali mbali wanaendelea  kupambana na maradhi hayo na kuja kwa Taasisi hiyo itaendeleza jitihada za kumaliza ugonjwa huo hapa nchini.

Amefahamisha kuwa maradhi yasiopewa kipa umbele yanawathiri watu wengi duniani na hata kupoteza maisha hivyo wataendelea kushirikina na mashirika mbali mbali kuona kwamba maradhi hayo yakiwemo matende, Mabusha Minyoo yanaondoka kabisa hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi unayoshughulikia Maradhi yasiopewa kipaumbele ya nchini Uengereza Thoko Elphick  Pooley amesema taasisi yake imeungana na mashirika mbali mbali duniani katika kukabiliana na maradhi yasiopewa kipaumbele katika nchi za Afrika.

Amesma watasaidia Zanzibar katika kupambana na maradhi hayo ili kuweza kuyaondosha kabisa kwa kuwapatia taaluma wafanyakazi wake sambamba na kuwapatia fedha kwa lengo la kuondosha maradhi hayo hapa nchini.

Loading