Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Itaendelea kudhibiti bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya Mwanaadamu

WIZARA ya Afya Zanzibar kupitia Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi itaendelea kudhibiti bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya mwanadamu ili kuondokana na maradhi mbali mbali yakiwemo yasioyakuambukiza. Akizundua Bodi ya Pili ya ushauri ya Wakala Chakula, Dawa na Vipodozi ZFDA Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kupatikana kwa Bodi hiyo kutaengeza ufanisi wa […]

WIZARA ya Afya Zanzibar inatarajia kufanya utafiti maalum wa kitaifa wa viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza (NCD Steps Survey)

WIZARA ya Afya Zanzibar inatarajia kufanya utafiti maalum wa kitaifa wa viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza (NCD Steps Syrvey) ifikapo Septemba 9 mwaka huu ikiwa na lengo la kuandaa mikakati ya kuona maradhi hayo yanapungua. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Naibu waziri wa Afya Zanzibar, Hassan Khamis Hafidh, alisema, utafiti huo utagusa jumla ya kaya […]

Wizara ya Afya Zanzibar yatiliana saini mkataba wa mashirikiano na Taasisi ya Mkapa Foundation

WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa mashirikiano baina ya Benjamini Mkapa Foundation wa kuimarisha sekta ya afya hapa nchini. Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Amour Suleiman Mohamed amesema mkataba huo utaimarisha ushirikiano wa utaoji wa huduma za afya katika nyanja tofauti ikiwemo ya rasilimali watu. Amesema Benjamini Mkapa Foundation imekuwa […]

Waziri wa Afya Zanzibar amepokea msaada wa vifaa vya Wamama Wajawazito kutoka Vodacom Tanzania Foundation

WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kuja kwa mradi wa Mmama utasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi hapa nchini. Akizungumza na waandhishi wa wa habari kuelekea uzinduzi wa kupatiwa vifaa vya mama wajawazito kupitia mradi wa Mmama vilivyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation ambavyo vitatolewa huko Kizimkazi na Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa […]

Loading