Wizara ya Afya Zanzibar yatiliana saini mkataba wa mashirikiano na Taasisi ya Mkapa Foundation

WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa mashirikiano baina ya Benjamini Mkapa Foundation wa kuimarisha sekta ya afya hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Amour Suleiman Mohamed amesema mkataba huo utaimarisha ushirikiano wa utaoji wa huduma za afya katika nyanja tofauti ikiwemo ya rasilimali watu.

Amesema Benjamini Mkapa Foundation imekuwa ikishirkiana na Serikali katika kuvitekeleza vipa umbele katika sekta ya afya ambavyo vimejumuishwa kwenye mkataba huo vya kuhakikisha wizara ya afya inafanya vizuri katika kufikia malengo ya utoaji wa huduma wa afya.

Amefahamisha katika mkataba huo utahakikisha suala la rasilimali watu wa kutoa huduma vituo vya afya, mafunzo kwa wafanyakazi wake, mfuko wa Bima ya afya kwa wote, vifaa tiba, pamoja na kuimarisha huduma za afya ya mama na watoto ili lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi linafikiwa.

Amesema katika kuimarisha huduma za afya Wizara itafanya kazi kwa pamoja na Benjaminin Mkapa Foundation ya kuhakikisha inapata fedha za kutosha pamoja na kuwa na mindombinu imara ili kuweza kutoa huduma bora za Afya na kutekeleza yote waliyokubaliana.

Kwa upande wake wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa Foundation Dkt Ellen Mkondya Senkoro amesema mkataba huo utaimarisha utoaji wa huduma za afya kwa upana zaidi kwa Zanzibar ambayo ni wa miaka mitatu.

Amefahamisha mkataba huo utasaidia katika masuala mazima ya rasilimali watu, mabadiliko katika sekta ya afya, kutoa ushauri na kuimarisha mifumo ya sekta ya afya pamoja Digital Health na njia za ubunifu wa kuimarisha huduma.

Amesema Benjamini Mkapa Foundation itahakikisha inashirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar kutekeleza kazi mbali mbali walizokubaliana katika mkataba huo ili huduma zinazotolewa ziwe zenye ubora kwa wananchi wa Zanzibar

Loading