Wizara ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa Gari kutoka kampuni ya CRJE

WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea Gari kutoka kampuni ya ujenzi CRJE yenye thamani ya zaidi ya milioni 70 ambayo itatumika kwa ajili ya ufuatiliaji wa miradi ya  wa Hospitali mpya  za Wilaya na Mkoa hapa nchini.

Akipokea Gari hiyo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amesema Gari hiyo ni kwa mujibu wa Mkataba wa kukamilisha ujenzi wa hospitali walizopewa kujenga ambazo ni Chumbuni, Mbuzini na Hospitali ya Jitimai.

Amesema Gari hiyo imekabidhiwa kwa Wizara ya Afya kwa mujibu wa Mkataba ambao umeeleza kuwa mara unapomaliza kujenga Hospitali hizo unakabidhi gari kwa ajili ya ufuatiliaji wa majengo hayo huku akisisitiza kuwa wataendelea kuziangalia Hospitali hizo kasoro zitakazojitokeza kwa kipindi cha mwaka mmoja na kampuni iweze kuzitatua.

Ameipongeza Kampuni ya CRJE kukamilisha kwa wakati Hospitali hizo na kujenga majengo yenye ubora na kuyataka Mkampuni mengine kufuata mikataba ya ujenzi wa hospital hizo na kukitaka Kitengo cha ufundi ambacho kinapewa gari hiyo kuitumia vyema gari hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Amour Suleiman Mohamed amesema Kampuni ya CRJE imepewa tenda ya kujenga Hopitali tatu za Wilaya ambazo zimekamilika kwa wakati na tayari zishakabidhiwa kwa Wizara ya afya na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Amefahamisha kuwa Hospitali hizo bado zipo kwenye uangalizi wa Kmpuni ya CRJE kwa kipindi cha mwaka mmoja kuangalia kasoro zitakazojitokeza na kuzipatia ufumbuzi kwa mujibu wa Mkataba na ni   miongoni mwa kampuni zilizoweza kufanikisha mkataba wao kwa ufanisi mkubwa.

Nae Mwakilishi kutoka Kmapuni ya CRJE Shi Yan amesema wamefanya kila jitihada kuona kuwa wanamaliza ujenzi huo kwa wakati na kuiomba Serikali kuzidi kuwaamini katika kutekeleza miradi mbali mbali hapa nchini.

Loading