WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini Mkataba wa mashirikiano na MSD

WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini Mkataba wa mashirikiano na Bohari kuu ya dawa Tanzania MSD wa kuimarisha masula mazima ya huduma za dawa hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Amour Suleiman Mohamed amesema Mkataba huo ni muendelezo wa makubaliano ambayo yapo kwa muda mrefu kati ya Bohari kuu wa dawa Zanzibar na Bohari kuu ya Dawa MSD ya    kuimarisha huduma za dawa kuwa zenye ubora zaidi nchini Tanzania.

Amesema makubaliano hayo yamehusisha katika masula mazima ya utaalamu wa kuwajengea uwezo wafanyakazi, kuimarisha miundombinu ya Bohari kuu za Dawa kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara, uhifadhi wa dawa pamoja na vifaa Tiba pamoja na matumizi ya Tehama.

Aidha amefahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar   kupitia Wizara ya Afya   imeweka vipa umbele vya kuimarisha huduma za afya vikiwemo masula mazima ya dawa kama ilivyoanishwa katika mkataba huo.

Amesema Wizara ya Afya kupitia Bohari Kuu ya dawa itaendelea kushirikiana na MSD katika kutoa huduma bora za dawa hasa katika maeneo ya mifumo kwenye uagizajia dawa,  Vifaa tiba, uhifadhi na ununizi wa dawa pamoja na kutafuta Fedha kwa ajili ya kuwa na dawa za kutosha ziweze kusaidia hapa nchini.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari kuu ya Dawa MSD Mavare A. Tukai amesema MSD na Wizara ya Afya wanamahusino ya kihistoria ambayo yamewezesha kuimarisha huduma za dawa kwa kubadilishana uzoefu, wataalamu pamoja na kusadiana kwa karibu pale panapotokea dharura.

Amesema mkataba huo utazidisha ushirkiano ambao utarahisha kufanya kazi kwa pamoja zaidi hasa katika masuala mazima ya mifumo ukizingatia kuwa mahitaji ya dawa na vifaa tiba yanazidi kuongozeka nchini Tanzania na kuahidi kuendeleza ushirikiano na Zanzibar kwa kuleta huduma zenye kwenda na wakati.

Katika hatua nyengine Wizara ya afya imetiliana saini mkataba wa makubaliano na Afrika Relief ya Nchini Marekani na Local Potential Enhancing ya Canada wenye lengo la kusaidia utoaji wa huduma za maradhi macho hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Amour Suleiman Mohamed amesema Mkaba huo utahusisha utaoji wa vifaa kwa ajili ya uchunguzi wa maradhi ya macho, kufanya upasuaji na kusimamia wagonjwa waliogundulika na maradhi ya jicho.

Amesema wananchi wapatao mia mbili wataweza kunufaika na mpango huo kwa Unguja na Pemba ambapo mia moja watahudumiwa Unguja na mia moja watapatiwa huduma kisiwani Pemba wa kufanyiwa matibabu wa mtoto wa jicho.

Aidha alifahamisha matibabu yatatolewa kupitia kwa madaktari bingwa kutoka taasisi hizo kwa kushirikina na madaktari wa hapa nchini na amewashukuru madaktari hao kuja kutoa huduma hizo na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuondosha matattizo mbali mbali ya maradhi ya macho.

Loading