Serikali ya Zanzibar imedhamiria kuhakikisha huduma bora za Afya zinapatikana muda wote kwa wananchi

Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Husein Ali Mwinyi imedhamiria kuhakikisha wananchi wa visiwa vya Zanzibar wanapata huduma bora za afya muda wote.

Hadi sasa tayari ujenzi wa hospitali 10 za Wilaya kwa Unguja na Pemba na moja ya Mkoa karibu umekamilika ambapo bado kufunga au kuweka baadhi ya vifaa. Baadhi ya hospitali hizo tayari zinatoa huduma mbalimbali za matibabu na nyengine zikiwemo za maabara, mionzi, huduma ya dharura, huduma za uzazi na huduma nyengine. Hatua hiyo imekuja baada ya Mhe. Rais, Dkt Mwinyi kuona kwamba wananchi wanapata huduma za uhakika kwa ukaribu na zenye ubora katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Kwa upande wa Hospitali ya Mnazi Mmoja inatarajiwa kukarabatiwa upya na kuwekwa mifumo mizuri zaidi na vifaa tiba vipya vya kisasa. Ujenzi wa hosptali hiyo utaanza Mwezi Januari mwaka 2024. Hospitali hiyo itakapokamilika matibabu yakayotolewa hospitalini hapo yatakuwa bora zaidi na ya yatakuwa ya hadhi au kiwango cha kibingwa zaidi.

Imetolewa na:
-Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Afya, Zanzibar

Loading