Ziara ya Watendaji wa Wizara ya Afya katika Hospitali za Mkoa na Wilaya.

WATENDAJI wa Wizara ya Afya Zanzibar wamefanya ziara maalumu katika Hospitali ya Mkoa na za Wilaya mara ya baada ya kukabidhiwa rasmi kutoka kwa wakandarasi na kuanza zoezi la uwekwaji wa vifaa.

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema zoezi la uwekaji wa vifaa katika Hospitali ya Mkoa Lumumba linatarajiwa kuanza leo na huku kwa upande wa hospitali za Wilaya Magogoni na Chumbuni tayari uwekaji wa vifaa umeshaanza na wanatarajia kumaliza hivi karibuni na kuanza kazi hivi karibuni

Amefahamisha kuwa kwa upande wa Hospitali ya Lumumba inatarajiwa kuanza kazi zake kwa majaribio mwezi wa Septemba mwaka huu  na kufunguliwa rasmi mwezi wa kumi na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Amesema katika ziara walioifanya wameweza kubaini kasoro ndogo ndogo za kiufundi na kuwataka wakandarasi kuzitatua kasoro hizo na kuweza kukamilisha kabla ya ufunguzi wa Hosptali hizo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amesema hatua za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa Lumumba na Wilaya umekamika na wapo katika matayarisho ya kuzifungua hospitali hizo kwa lengo la kuwahudumia wananchi.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga katika masula mazima ya kutoa huduma kwenye hospitali hizo ambapo wataalamu pamoja na vifaa tiba vitawekwa ili kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu.

Katika ziara hiyo watendaji wa Wizara ya Afya wameweza kutembela Hospitali ya Mkoa Lumumba, Hospitali ya Wilaya Magogoni pamoja na Hospitali ya Chumbuni.

Loading