Wizara ya Afya Zanzibar yapokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Diaspora

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na wananchi wanaoishi nnje ya nchi Diaspora kwa lengo la kuimarisha huduma za Afya hapa nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui huko Hospitali ya Wilaya Kitogani wakati alipopokea msaada wa vifaa tiba na dawa kwa  watanzania wanaoishi Marekani Diaspora  wenye thamani ya Dola laki tatu ambavyo vitatumika katika Hospitali ya Wilaya Kitogani na kitengo cha Meno Mnazi mmoja.

Amefahamisha mbali na msaada huo wa watanzania wanaoishi Nchini Marekani pia wamekuja na diaspora wataalamu wa magonjwa mbali mbali kutoka Nchini Kenya, Lusoto  na nyenginezo  kwa lengo la kutoa huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya Kitogani.

Amefahamisha kuwa diaspora wakitanzania hawajaitupa nchi yao wanasaidia katika nyanja tofauti ikiwemo kuja kuwahudumia wananchi wa Zanzibar ambapo kutawawezesha kuwapatia taaluma wataalamu wa Zanzibar pamoja na wao  kujifunza na kuwataka waendeleze jitihada hizo kutokana na fursa walizonazo.

Kwa upande wa kiongozi wa watanzania wanaoishi nchini Marekani Asha Nyanganyi amesema wamekuja na timu ya Madaktari na wauguzi na wataalamu wengine wa afya wakishirikina na wataalamu kutoka nchi nyengine ambao watatoa huduma mbali mbali za afya zikiwemo za moyo,kisukari, huduma za maabara na magonjwa mengine.

Amefahamisha kuwa wataendelea kuisadia nchi yao katika kuwapatia huduma mbali mbali zikiwemo za afya na kubadiliasha uzoefu ili kuweza kuwahudumia wananchi wa Tanzania.

Nae Daktari dhamana wa Hospitali Lwanyumba Joram Lwegasila ya Wilaya Kitogani Dkt ameshukuru Serikali Kupitia Wizara ya Afya kwa hatua ya kuja kwa wataalamu hao ambao wamewezesha kusaidia katika kuwapatia huduma wananchi pamoja na watalaamu wa hospitali hiyo kupata ujuzi.

Loading