NIMRI kufanya utafiti wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa ushirikiano wa WHO na Serikali ya Tanzania

SERIKALI ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na  Shirika la Afya ulimwenguni WHO inakusudia kufanya Utafiti wa Viashiria vya Magonjwa yasiombukiza kote nchini ili kuweza kutambua ukubwa wa magonjwa hayo

Akizindua utafiti wa kitaifa wa viashiria vya magonjwa yasiombukiza huko Dodoma Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kutokana na ongezeko la maradhi yasiombukiza hapa nchini Serikali zimeamua kufanya utafiti huo utakaoendeshwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa maradhi ya Binaadamu NIMRI.

Amesema utafiti huo utakuwa ni wapili ambapo uutafiti uliopita ulifanyika mwaka 2011 kwa Zanzibar na 2012 kwa Tanzania bara ambapo kwa utafiti huu  unaotarajiwa kufanyika Tanzania nzima utakaoanza  ta mwezi wa nane mwaka huu utawajumuisha watu kuanzia miaka 18 hadi 69.

Amesema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya ulimwenguni WHO za mwaka 2020 vifo milioni 41 vya magonjwa yasiombukiza vilitokea sawa na asilimia 71 ya vifo vyote na milioni 57 walifariki mwaka 2016.

Amefahamisha kwa upande wa Tanzania takwimu zinaonesha kuwa tatizo la magonjwa yasiombukiza yanasababisha vifo asilimia 33 ya vifo vyote na takwimu zinazokusanywa katika vituo vya kutolea huduma za afya zinaonesha ongezeko kubwa la magonjwa yasiombukiza.

Aidha amefahamisha kuwa wagonjwa wengi wanaohudhuria vituo vya kutolea huduma Tanzania ni wa magonjwa ya shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya mfumo wa hewa na magonjwa mengine.

Ameitaka kamati inayofanya utafiti huo pamoja na wadau wa maendeleo kushirikiana wakati wa utekelezaji wa utafiti huo kwa lengo la kuzuiya na kudhibiti magonjwa yasioambukiza huku akiwataka kufanya tafiti za magonjwa hayo kila baada ya muda mfupi na sio kukaa kwa kipindi kirefu kunasababisha athari kubwa kwa jamii.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Taifa ya utafiti wa maradhi ya binaadamu NIMRI Profesa Said Aboud amesema takwimu zitakazokushanywa kupitia utafiti wa viashiria vya maradhi yasiombukiza zitatumika kama dira ya kuongoza kuelekea kutengeneza mikakati yenye ushahidi ili kuweza kuimarisha afya za watanzania.

Amefahamisha kuwa kwa kuelewa viashiria vya  hatari vya magonjwa  yasiombukiza vikiwemo kama vile utumiaji wa tumbaku, unywaji wa pombe kutofanya mazoezi , ulaji usiofaa kutawezesha kubuni mbinu ambazo zitasaidia kuondokana na tatizo hilo na kuwa na takwimu sahihi na kuweza kukabilina na magonjwa yasiombukiza.

Kwa upnde wa Mwakilishi kutoka Shirika la Afya ulimwenguni WHO Dkt Alphancne Nanai ambae amesema vifo kumi vinavotokea dunini kote vifo saba vinasababishwa na magonjwa yasiombukiza.

Amefahamisha kuwa watu wengi wanasumbuliwa na magonjwa yasiombukiza bila ya kujijua kutokana na kuwa ugonjwa huo hauna dalili za moja kwa moja hivyo  utafiti huo utasaidia kutambua ukubwa wa magonjwa ya maradhi yasiombuliza hapa nchini.

Nae Mkurugenzi kinga na Elimu ya Afya Dkt Salim Slim amesema kuwa ushirikiano wa kufanya utafiti huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuweka   misingi mizuri ya kuondosha tatizo hili na kundokana na vifo vya mapema pamoja na kukuza uchumi wa watanzania.

Mapema Mganga Mkuu Wizara ya afya Tanzania Bara Profesa Tumaini Nagu amesema kumeundwa kamati ya kitaalamu na ya kiushauri ambayo imejumuisha wataalamu kutoka Tanzania bara na visiwani lengo ni kufanikisha utafiti huo na kuleta matokeo mazuri hapa nchini.

Loading