Waziri wa Afya Zanzibar akutana na Madaktari wa Meno kutoka Oman

WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kuja kwa madaktari wa maradhi ya meno kutoka Oman kumesaidia kwa kiasi kikubwa kufanya uchunguzi na matibabu kwa wananchi wa Zanzibar.

Amesema wananchi wengi hasa watoto wanasumbuliwa na maradhi ya meno kutokana na kula vyakula kwa wingi vya sukari na vikali ambapo kunasababishwa kwa kiasi kikubwa kuharibu meno

Waziri Mazrui ameyaeleza hayo huko Bwejuu alipotembelea kambi ya uchunguzi na matibabu ya meno iliyofanywa na Chuo kikuu cha maneno cha nchini Oman kwa kushirikiana na madaktari wa meno hapa nchini.

Amefahamisha kuwa afya ya meno ni muhimu sana kwa binaadamu hivyo amewataka wananchi kuyatunza meno ili kuweza kuondokana na matatizo ya maradhi ya meno ambayo yamekuwa yakiwasumbua watu wengi kutokana na kutotunza afya ya kinywa na meno.

Amekishukuru chuo kikuu cha meno cha nchini Oman kwa kuja kutoa huduma hiyo hapa nchini katika maskuli mbali mbali ameomba kuendelea kusaidia Zanzibar kutoa huduma hiyo  pampja na taaluma kwa madaktari na kutaoa taaluma ya afya ya kinywa na meno  kwa wanafunzi ambao ndio tegemeo la hapo baadae.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo Kikuu cha meno nchini Oman Profesa Nutayla Said Al Harthy amesema katika uchunguzi walioufanya kwa wanafunzi wa skuli ya Charity Bwejuu watoto wengi wamewagundua na matatizo ya meno yakiwemo kutobaka ambayo husababishwa na kula vyakula vyenye sukari kwa wingi.

Amefahamisha kuwa Chuo Kikuu cha meno cha nchini Oman kitaendelea kuja  Zanzibar kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii,  kujifunza pamoja na  kutaoa elimu kwa madaktari pamoja na elimu ya afya ya kinywa na meno kwa wanafunzi wa maskuli mbali mbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo Kikuu cha meno cha Nchini Oman Profesa Mohamed Al Ismail amesema kufanyika kwa kambi za uchunguzi na matibabu ya maradhin mbali mbali ikiwemo ya meno kunasadia kutambua magonjwa  na kuyapatia matibabu kwa haraka kwa jamii hasa wa vijijini.

Amefahamisha mbali na kuibua wagonjwa pia wafanyakazi, wanafunzi wanapata faida kubwa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu wa kitabibu.

Nae Daktari wa Meno kutoka Hosptali ya Mnazimmoja Dkt Sumaiya Said Aboud amesema katika kambi hiyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka Oman wameweza kuwachunguza watoto wa skuli ya charity ya Bwejuu,  na wamegundua matatizo ya meno kwa wanafunzi yakiwemo ya kutoboka kwa meno ambao walipewa matibabu.

Loading