Ziara ya Mh.Waziri kwenye vituo vya Afya Wilaya ya Kati na Mjini

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema inakusudia kuimarisha huduma za afya ya msingi kwa kuweka mindombinu yenye ubora zaidi  na wananchi waendelee kupata matibabu bila ya usumbufu.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui katika muendelezo wa Ziara yake  ya kutembelea vituo vya afya aliyofanya Wilaya ya Kati na Mjini ya kuangalia miundombunu na changamoto zinazowakabili wafanyakazi.

Amesema katika kuimarisha afya ya msingi Wizara imepanga kuvifanyia matengenezo makubwa vituo mbavyo vitahitajia matengenezo na kuvijenga upya vituo ambavyo ni vya zamani sambamba na kuwekwa vifaa tiba dawa pamoja na rasilimali watu.

Aidha alisema katika vituo vya Afya, watahakikisha kuwa huduma za afya ya mama na mtoto zinaimarishwa na kuendelea kuongeza jitihada na ndani ya miaka minne ya kuwapa huduma zenye ubora Zaidi.

Amefahamisha kuwa kuimarisha huduma katika afya ya Msingi kutasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kupata huduma nzuri ndani ya wakati unatakiwa na kuweza kupunguza msongamano katika Hospitali ya rufaa mnazimmoja.

Amesema watahakikisha wanarekebisha mapungufu yote yautendaji kazi katika vituo vya afya kwa kuanzia katika masula ya uagizaji wa dawa ziendane na mahitaji halisi ya wagonjwa pamoja na mambo mengine.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt Fatma Kabole amesema kuwa katika kuimarisha huduma za afya vituoni ni lazima wafanyakazi wafanye kazi  kwa bidii kwa kuzingatia maadili ya kazi ikiwa na pamoja na kuwa na leseni yakufanyia.

Aidha amewashajihisha wahudumu wa Afya wa kujitolea CHV kuendelea kushirikiana na wafanyakazi vituo vya Afya kuwapeleka watu wenye matatizo mbali mbali wakiwemo mama wajawazito na watoto.

Kwa upande wa Daktari dhamana Wilaya ya Mjini Ibrahim Makame amesema kufuatia ziara iliyofanyika katika vituo vya afya Unguja na Pemba watahakikisha wanabadilika kiutendaji na kutoa huduma zenye ubora Zaidi hapa nchini

Amefahamisha licha ya kufanya kazi kwa bidii kubwa bado wanakabiliwa na changamoto ya fedha za kuendeshea kazi zao vifaa tiba na rasilimali watu na kupelekea utendaji wa kazi usioridhisha.

Loading