WIZARA ya Afya Zanzibar Kuimarisha mashirikiano yake na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendeleza mashirikiano yake na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO katika kuimarisha huduma za Afya hapa nchini.

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema hayo huko ofisini kwake wakati alipomkaribisha Mwakilishi Mkaazi mpya wa Shirika la Afya ulimwenguni nchini Tanzania alipofika kwa kujitambulisha.

Amesema WHO inafanya kazi kubwa hapa nchini ya kuhakikisha kuwa wanapambana na magonjwa mbali mbali yakiwemo yakuambukiza na yasioambukiza pamoja na kuwajengea uwezo wafanyakazi wake.

Amefahamisha kutokana na ongezeko la hali ya maradhi yasiombukiza NCD amemuomba mwakilishi huyo kuzidi kushirikiana kwa karibu zaidi   katika kuwapatia miongozo mbali mbali ya kukabiliana na magonjwa hayo, kuwajengea uwezo wafanyakazi wake pamoja na vifaa tiba.

Aidha alifahamisha kuwa  Shirika hilo limeweza  kusaidia kwa kiasi kikubwa katika masula mazima ya chanjo mbali mbali ikiwemo ya uviko 19, mpango wa chanjo ya kipindupindu ambayo mkakati wake ni wakutomeza kabisa  kipindupindu mwaka 2021/27 hapa Zanzibar.

Amesema ushirikiano huo uliopo baina ya Serikali kupitia Wizara ya Afya  utazidi kuendelea   na mipango  itatekelezwa ili wananchi wa Zanzibar waomdokane na magonjwa.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO nchini Tanzania Charles Sego Moses amesema ataendeleza Mashirikiano na Zanzibar kupitia Wizara ya Afya ya  kuendeleza kazi na mipango mikakati kupitia Shirika hilo.

Amesema katika utekelezaji wake wa kazi nchini Tanzania atahakikisha masuala mbali mbali yanatekelezwa ikiwemo chanjo, kukabiliana na majanga na magonjwa mbali mbali.

Loading