Wizara ya Afya Zanzibar Kuendeleza ushirikiano na UNICEF

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto Duniani UNICEF katika kuimarisha huduma za Afya hapa nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui wakati alipofanya mazungumzo na Mwakilishi mpya wa taasisi ya hifadhi ya watoto wa shirikika la umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto dunini nchini Tanzania aliyefika kujitambulisha.

Amesema UNICEF inafanya kazi kwa ukaribu sana na Wizara ya afya katika kuwasaidia mama wajawzito na watoto pamoja na mambo mengine, ambapo wameweza kutekeleza miradi mbali mbali ya uimarishaji huduma hapa nchini.

Aidha ameliomba Shirika la UNICEF kuendeleza misaada yao katika sekta ya  Afya hasa uimarishaji wa huduma ya msingi kwa kuwapatia vifaa tiba dawa kwa lengo lakupunguza vifo vitonavyo na uzazi.

Amefahamisha wataendeleza mashirikiano na Shirika hilo  na kuendelea kusifu hitihada kubwa zinazofanywa za kuendelea na kuthamini  misaada yao  ambayo imekuwa ikiunga jitihada za Serikali.

Kwa upande wake mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Elke Wisch ameshukuru ushirikiano uliopo hapa nchini katika nyanja tofauti ikiwemo sekta ya afya na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.

Amesema UNICEF itaendelea na dhamira yake ya kuimarisha huduma mbali mbali kwa jamii ya wazanzibari ikiwemo kuimarisha sekta ya Afya, Elimu, maji safi na salama na afya ya mazingira.

Loading