Zanzibar na China kuendeleza ushirikiano katika sekta ya Afya

Zanzibar na China zimetakiwa kuimarisha ushirikiano uliopo ili kuweza kuzalisha madaktari bingwa wa upasuaji wa kutumia matundu madongo kwa magonjwa mbalimbali hapa Zanzibar.

kauli hiyo imetolewa na Dkt. Mwanabaraka Saleh Mkurugenzi hududma za upasuaji Hospitali ya Mnazi mmoja amesema  ujio Madaktari kutoka china umesaidia Hospitali ya Mnazi mmoja kupata Madaktari bingwa sita wa upasuaji kwa kutumia matundu madogo.

Dkt Mwananbaraka amesema kwa wakati huu ambao Serikali inaimarisha  Sekta ya Afya ni wakati sasa Zanzibar kuwa na Madaktari bingwa wa upasuaji kupitia matundu madogo (laparascopy)

Dkt Rashid Masoud Said ni miongoni mwa waliopata mafunzo ya upasuaji kutumia matundu madogo amesmea ushirikiano wa zanzibar na china umezidi kuleta fadia kwenye sekta ya afya kwa kupatiwa mafunzo na madaktari wanaokuja kutoka china ambapo wanafanikisha kazi mabali mbali hospitalini hapo.

Dkt  Jiang Guoqing ni Kiongozi wa timu ya 33 ya madaktari kutoka china amesema kuwa wanayofuraha kuona madaktari wazawa wanafanya vizuri katika upasuaji wa kutumia matundu madogo jambo ambalo linaleta faraja katika mashirikiano ya nchi hizi mbili.

Loading