WIZARA YA AFYA IMEPOKEA MSAADA WA FEDHA KUTOKA CHINA

WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa vifaa mballimbali vikiwemo vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia tisa na 20 kutoka hospitali ya jiji la Jiangsu China vitakavyotumika katika Hospitali ya Mnazimmoja na Abdalla Mzee Pemba.

Msaada huo umepokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Habiba Hassan Omar na kutia saini mkataba wa makabidhiano, ambapo amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuthamini ushirikiano na misaada kutoka China ambayo inasaidia sekta ya afya.

Kaimu Balozi mdogo wa China Zanzibar Zhang Ming na Rais wa Hospitali ya Jiangsu, Dkt. Shu Yusheng wameahidi kuwa China itaongeza kiwango cha juu cha misaada kwa Zanzibar ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta ya afya.

Hospitali ya Jiangsu imekuwa ikileta timu ya madaktari Zanzibar ambapo hadi sasa ni timu ya 33 ya madaktari inatoa huduma katika hospitali za Zanzibar.

Loading