Wananchi wametakiwa kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto

Wananchi wametakiwa kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao wanaohitaji huduma hiyo katika hospitali za Unguja na Pemba.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Habiba Hassan Omar katika bonanza la uchangiaji damu katika viwanja vya Mapinduzi Squre Kisonge.

Amesema Zanzibar inahitaji unity za damu 13 elfu kwa kipindi cha miezi mitatu ili kuweza kusaidia watu wenye mahitaji jambo ambalo kwasasa limekuwa halifikiwi na kusababisha upungufu wa damu katika hospitali za Serikali na binafsi.

Mkurugenzi Idara ya Uuguzi na Ukunga Mwananisha Juma Fakii amesema kuwa ukosefu wa damu ni moja ya sababu inayosababisha vifo vya mama na mtoto Zanzibar.

Amesema vifo vya mama na mtoto vimekuwa vikiongezeka kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa damu hivyo ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliojitokeza kuchangia damu wamewaomba wananchi kupenda kuchangia damu ili kusaidia watu wenye mahitaji damu.

Loading