Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Mazrui amesema mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wete Pemba unatarijiwa kuanza hivi karibuni

WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wete Pemba unatarijiwa kuanza hivi karibuni mara baada ya kupatikana mshauri elekezi.

Waziri Mazrui ameyaeleza hayo huko ofisini kwake alipofanya mazungumzo na Balozi umoja wa nchi falme za kiarabu UAE aliyepo Zanzibar yaliyohusina na maendeleo ya ujenzi wa mradi wa hospitali ya Wete kisiwani Pemba na miradi mengine.

Amesema tayari mshauri elekezi wa ujenzi wa hospitali hiyo ameshapatikana na baada ya wiki mbili atafika kisiwani Pemba kukabiziwa mradi huo kwa kuanza hatua ya ujenzi.

Amesema hatua ya ujenzi huo ni muhimu sana kisiwani humo ambapo mara ya kukamilika ujenzi huo wananchi watapata huduma za kisasa katika hospitali hiyo.

Amefahamisha  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikina na umoja wa nchi za Falme za Kiarabu UAE ambao umenaza kwa mika mimgi na kumetekelezwa   miradi mbali mbali ikiwemo miradi sita hapa nchini ambao ni  ujenzi wa hospitali ya Makunduchi, Skuli.

Kwa upande wake Balozi wa umoja wa nchi za Falme za Kiarabu UAE aliyepo Zanzibar Saleh Ahmed Alhemeiri amesema atahakikisha kuwa ujenzi wa Hospitali ya Wete unaanza kufanyika hivi karibuni.

Amesema  wataendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar sambamba na  kutekeleza miradi yote ikiwemo ya sekta ya afya na elimu.

Loading