WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa dawa kutoka Shirika la Maendelo HIPZ

WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa dawa kutoka Shirika la Maendelo HIPZ zenye thamani ya shilingi milioni mia sita na hamsini ambazo ni za maradhi ya kisukari, Presha na magonjwa ya akili na zitatumika Hospitalini na Vituo vya Afya.

Akipokea msaada huo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amesema Maradhi ya Presha, Kisukari na Ugonjwa wa akili yamechukua nafasi kubwa katika kuwasumbua wananchi wengi hapa Zanzibar na kupatikana kwa dawa hizo kutasaidia kuimarisha afya za wenye maradhi hayo.

Amesema Taasisi ya HIPZ imekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya afya ambapo mbali na msaada huo, wanasadia katika kuimaridha afya za mama na mtoto, huduma za Maabara katika Kituo cha Afya Makunduchi na huduma nyengine.

Ameitaka Bohari kuu ya dawa kuhakikisha dawa hizo haziibiwi na zinawafikia walengwa na kufanya ufuatiliji wa makusdi katika vituo vya Afya na kuzisambaza kwa wakati.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mipango kutoka HIPZ Simon Kuhnert amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inachukua jitihada  kubwa ya kuhakikisha kuwa Afya kwa wote inafikiwa  kwa kuimarisha huduma za afya hapa nchini.

Amesema HIPZ imeweza kuunga jitihada za Serikali kwa kutekeleza  mambo mbali mbali ya kuimrisha huduma za Afya ikiwemo huduma za afya,  ya mama na mtoto, huduma za Mabara

Akitoa shukurani baada ya kupokea msaada wa dawa hizo Mkurugenzi bohari kuu ya dawa Zanzibar Abdul halim Mohd Mzale amesema dawa hizo ni dawa ambazo zinahitajika katika utoaji wa huduma za afya na amelishukuru shirika la hipz kwa msaada huo.

Loading