Wizara ya afya yapokea msaada wa Mashine ya Methadone

WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa mashine ya kurahisishia utoaji ya matibabu ya methadone kwa waraibu wa dawa ya kulevya kutoka Serikali ya Marekani kupitia Amref Health Africa Tanzania yenye thamani ya shilingi milioni themanini na nne.

Akipokea msaada huo Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema msaada huo utasaidia katika kurahisha upatikanaji wa huduma kwa waraibu wa dawa za kulevya wakati wanapofika kupata huduma ya methadone hapo kituo cha Kidongochekundu.

Amefahamisha kuwa kuwekwa kwa mashine ya kupimia dawa ya methadone itawezesha kupunguza changamoto mbali mbali zikiwemo muda mrefu wa kuwahudumia waraibu, matumizi ya kutunza kumbukumbu katika karatasi, mzigo mzito wa watoa huduma pamoja na kutoa dawa kwa kukadiria.

Waziri Mazrui amewataka wafanyakazi kituoni hapo kuitunza mashine hiyo kwa lengo lakuwahudumia waraibu hao kwa uhakika na kwa muda mdogo, na kuwahakikishia kuwa Serikali kupitia Wizara ya afya itafanya kila jitihada ya kuhakikisha kuwa baada ya kumaliza kupata tiba ya methadone wanajishughulisha na kazi mbali mbali za kuwapatia kipato.

Aidha amelishukuru Shirika la Amref health Africa Tanzania pamoja na CDC kwa misaada yao mbali mbali katika sekta ya afya hasa katika masula mazima ya Ukimwi Homa ya ini kifua kikuu na ukoma na kuwataka kuendeleza misaada yao kwa Zanzibar.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka CDC Dkt Nyagonde Nyagonde amesema Tanzania imeweza kwa kiasi kikubwa katika kuwahudumia waraibu wa dawa za kulevya na nchi mbali mbali zimekuwa zikija kujifunza namna ya kuwahudumia waraibu hao

Amefahamisha wanampango wa kusambaza huduma hizo katika maeneo mbali mbali nchini tanzania ili kuweza kupata huduma hizo kwa urahisi na  ukaribu na kuwataka wanajamii kuondosha unyanyapaa kwa waraibu hao ili tatizo hilo lisiweze kuendelea.

Nae Mkurugenzi wa Amref health Africa Tanzania Dkt Florence Temu ammesema tangu mwaka 2015 wameweza kuwafikia waraibu wapatao 1596 wameunganishwa katika huduma hiyo na jumla ya waraibu 840 wanaendelea kupata huduma ya methadone kila siku.

Amefahamisha waraibu wapato 82 wamefariki na wengine wamekimbia kutokana na sababu mbali mbali na kusema kuwa mashine hiyo itarahisisha upatikanaji wa huduma kwa urahisi mkubwa.

Kwa upande wake Hashim Ali Haji ambae alikuwa ni mraibu wa dawa za kulevya amesema kuja kwa mashine hiyo itawarahisishia kwa wahudumu wa kituoni hapo kutoa huduma kwa urahisi na kutunza kumbukumbu.

Aidha amewataka waraibu kutochanganya dawa za kulevya wakati wanapopatiwa huduma ambapo kuwasababishia kutopona na kupelekea athari mbali mbali za kimaisha na afya zao.

Loading