Wizara ya Afya Zanzibar itaendelea kuimarisha huduma za afya ya msingi

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema inakusudia kuimarisha huduma za afya ya msingi kwa kuweka miundo mbinu na vifaa vya kutosha ili wananchi wapate huduma kwa ukaribu na kuweza kupunguza msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui alipofanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya CRDB pamoja na viuongozi wa Wizara ya Afya wenye lengo la kuimarisha huduma za afya hapa nchini.

Amesema ili kuweza kutoa huduma nzuri kwa wananchi ni lazima uwe na miundo mbinu iliyo bora, vifaa tiba, wahudumu wenye uwezo pamoja na madawa ya kutosha katika mahospitali na vituo vya afya.

Ameuwelezea ujumbe huo wa Benki ya CRDB kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya wananchi kukimbilia katika hospitali kuu na kuacha kuianzia kupata matibabu katika vituo vya afya vilivyo karibu, na hiyo inatokana na kukosekana kwa huduma muhimu katika vituo hivyo zikiwemo vipimo na dawa.

Kwa upande wa Meneja wa Mahusiano kitengo cha Serikali wa CRDB Benki amesema kuwa lengo la kukutana na uongozi wa Wizara ya afya ni kuimarisha  huduma za afya  ikiwa na pamoja na kujenga kituo cha afya pamoja na vifaa tiba.

Amesema kikawaida Benki hiyo inapata faida ya gawio linarudi kwa jamii  kulingana na mahitaj  ambapo kwa awamu hii imekuja kuimarisha huduma za afya kwa kuimarisha miundombinu, vifaa tiba pamoja na dawa.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Fatma Kabole ameulezea ujumbe huo kuwa kwa sasa mahitaji makubwa ni kuimarisha vituo vya afya vinavyotoa huduma ya uzazi ambavyo vinafikia 36 kwa Unguja na Pemba  na malengo makubwa ni kuweka  mindo mbinu iliyobora na vifaa vya kutosha ili wananchi wasipate usumbufu.

 

Loading