Wizara ya Afya imepokea msaada wa vifaa Tiba na dawa kutoka Marekani

WIZARA ya Afya Zanzibar imepokea msaada wa vifaa mbali mbali kutoka Taasisi Africa Relief and community Development ya Nchini marekani  na taasisi nyengine vyenye thamani ya Zaidi ya dola laki mbili.

Akipokea msaada huo Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema vifaa hivyo ni vifaa ni vya   kuwasaidia wagonjwa waliolazwa, vifaa vya sehemu ya upasuaji, vifaa vya maabara na dawa.

Amesema msaada huo utasaidia kuunga mkono jitihada za Serikali kupitia Wizara ya afya za kuimarisha huduma mahospitalini na vituo vya Afya.

Ameshukuru kwa msaada huo ambao umetolewa na taasisi tofauti na atahakikisha unawafikia walengwa na unatumiwa kama ilivyokusudiwa na kuwataka kuendeleza misaada yao kwa Zanzibar ili huduma ziwe zenye ubora Zaidi.

Kwa upande muakilishi kutoka Taasisi ya Tamam society Nassor Abdalla Rashid amesema wameshirikiana na Taasisi ya Africa Relief and community Development ya nchini Marekani kusaidia vifaa hivyo hapa nchini.

Amesema vifaa hivyo ni mwanzo  wa kusaidia hapa nchini na watahakikisha wanatafuta misaada mengine  Zaidi kwa lengo la kuimarisha huduma za afya hapa nchini.

Loading