Wiki ya Maabara

WATAALAMU wa Maabara nchini wametakiwa kufanya kazi kwa pamoja katika kufanya uchunguzi wa maradhi na bidhaa nyengine kwa lengo la kuimarisha afya za wananchi.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh wakati alipofanya ziara maalaumu ya kutembelea maonesho ya wataalamu wa maabara mbali mbali yaliyofanyika katika viwanja nya Mapinduzi Square Kisonge.

Amesema wataalamu wa Maabara wanajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanachunguza maradhi, na kufanya tafiti mbali mbali kwa lengo la kukabiliana na maradhi ya miripuko wakati yanapotokea.

Amefahamisha kuwa maabara zote zinatakiwa kushirikiana katika kuwahudumia wananchi na kuweza kukabiliana na maradhi mbali mbali yakiwemo yanayotaokana na wanyama, mimea, ili kuwa na bidhaa zenye ubora na viwango hapa nchini.

Amewataka wataalamu hao wa maabara kuendelea kufanya kazi zao kwa umakini mkubwa kutokana na kuwa tegemeo kubwa la kumapatia matibabu mgonjwa linaendena na majibu ya uchunguzi wa maabara.

Kwa upande wake mtaalamu wa maabara kutoka Baraza la wataalamu wa Maabara Time Hassan amesema wiki ya maabara huazimishwa duniniani kote kila ifikapo mwisho wa mwezi wa nne na lengo lake kubwa ni kutambua kazi za maabara na umuhimu wa maabara duniani kote.

Amesema ushirikiano wa maabara unaumuhimu mkubwa katika kuwahudumia wananchi ambapo kunawezesha kuwa na mifumo ambayo inasaidia kutoa majibu sawa na sahihi kwa mgonjwa na kuwataka wataalamu kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kujiendeleza kitaaluma Zaidi.

Nae Afisa uhamasishaji kutoka Mpango wa Damu Salama Zanzibar Omar Said Omar amesema katika kuadhimisha wiki ya wataalamu wa Maabara duniani wamehakikisha kuwa wanashiriki maonesho hayo kwa kutoa Elimu kwa wananchi sambamba na kuwataka wananchi kuchangia damu ili kuweza kusaidia wagonjwa wenye mahitaji.

Amefahamisha moja ya majukumu ya Mpango wa Damua salama Zanzibar baada ya uchangiaji wa damu ni kuhakikisha kuwa damu hiyo wanaifanyia vipimo na wataalamu wa maabara na baada ya hapo anapatiwa mgonjwa.

Loading